Jumanne, 11 Machi 2014

UZINDUZI WA KITABU CHA MAISHA NA HUDUMA YA ASKOFU MOSES KULOLA. SASA UNAWEZA KUKIPATA


Muonekano wa kitabu cha MAISHA NA HUDUMA YA MOSES KULOLA.
Jumapili ya jana kumekuwa na tukio kubwa na muhimu limefanyika katika kanisa EAGT Temeke, karibu na hospital ya Temeke ambapo kitabu cha MAISHA NA HUDUMA YA MOSES KULOLA. kimezinduliwa rasmi na sasa kitauza nchi nzima. Kitabu hicho kimeandaliwa na kina historia nzima ya marehemu Askofu mkuu Moses Kulola. jinsi alivyoanza huduma  na maisha ya huduma kwa ujumla. sio kitabu cha kukoka. 

Katika uzinduzi huo licha ya waumini wengi pamoja na watumishi wengi wa MUNGU kuhudhuria, walikuwepo pia mjane wa marehemu Kulola, Mama Kulola pamoja na Mchungaji Daniel Kulola ambaye ni mtoto wa askofu Kulola. 

N i kitabu kinachogusa sana maana huduma ya Askofu Kulola ilikuwa ni muhimu sana katika Kanisa la Tanzania na kupitia huduma hiyo maaskofu na wachungaji wengi  maarufu leo ni zao la uinjilisti wa askofu Kulola. BWANA YESU alitenda kazi yake kupitia  mtumishi wake Askofu Kulola  kwa kiwango  cha hali ya juu, Askofu Kulola alitembea Tanzania njia kuhubiri Injili  na hadi mwisho wa kufanya kazi ya MUNGU hapa duniani alikuwa anaongoza makanisa zaidi ya 4000.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za uzinduzi wa kitabu hicho
Maombi  tayari kwa kitabu kuzinduliwa



uzinduzi
Mama Kulola
Mama Kulola

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: