Jumapili, 30 Machi 2014

MGANGA WA KIENYEJI AKABIDHI TUNGULI ZAKE KANISANI ZACHOMWA MOTO.


Watu wanaojihusisha na masuala ya uganga na ushirikina wameendelea kujisalimisha kwa Yesu kufuatia maombi na neno linalohubiriwa katika kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Arusha. Hapo jana mwanadada Lightness amepeleka vifaa vyake vyote vya uganga na ushirikina kanisani hapo ili vichomwe moto kuashiria kwamba hataki kurudi tena katika kufanya vitendo hivyo.Mwimbaji nyota wa muziki wa injli nchini Jackson Benty akiimba katika ibada kanisani hapo ambapo pia huwa anaabudu.

Lightness akiwa amenyanyua vibuyu mbalimbali alivyokuwa akifanyia kazi zake.

Vifaa vya kazi vya Lightness katika picha.vyote vikawashwa moto na kuteketea.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Arusha Frank Andrew akimsikiliza dada huyo akizungumza.Wengi walitoka mbele kumpokea Yesu kwasababu ya kuona Mungu alivyotenda kuokoa washirikina.Baadhi ya umati wa waumini wa kanisa hilo. Picha Ufufuo Crew. 
 
 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni