Ijumaa, 28 Machi 2014

MHASHAM ASKOFU GODFREY MDIMI MHOGOLO WA KANISA LA ANGLICANA DAYOSISI YA CENTRA TANGANYIKA AFARIKI


Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Cetral Tanganyika
Askofu Godfrey Mhogolo wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Cetral Tanganyika amefariki dunia jana alhamisi Nchini Afrika Kusini alikokuwa amekwenda kwa matitabu..

Photo: REST IN PEACE  BISHOP MDIMI MUHOGOLO 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kanisa la Angilikana Dodoma jana, ilisema kuwa Askofu Mhogolo kabla ya kufikwa na mauti alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Milpark huko Johanesburg, Afrika Kusini. 

Askofu Mhogolo alikuwa askofu wa tano wa dayosisi ya Central Tanganyika na atazikwa katika viwanja vya kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Mjini Dodoma. 

Hata hivyo Mchungaji Michael Nchimbi alisema mipango ya mazishi inaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.

Askofu Mhogolo enzi za uhai wake.

BWANA alitoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni