Ijumaa, 12 Julai 2013

BONNKE KUFANYA MKUTANO MKUBWA MWEZI WA 8 HAPA TANZANIA

Mhubiri wa injili wa kimataifa Reinhard Bonnke anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa injili jijini Dar. mkutano huo utakaoanza tar 21-25/08/2013. mkutano huo mkubwa unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya nje ya uwanja wa taifa. taarifa zilizoifikia blog hii maandalizi mbalimbali zimeshaanza ikiwapo Maombi, kikundi cha kusifu na kuabudu, watu wa matangazo, wasimamizi wa wahudumu na idara mbalimbali. Muandaaji mkuu wa mikutano hiyo ukanda wa africa alisha wasili hapa tangu wiki iliyopita ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, kumekuwa na vikao vya mara kwa mara vya wachungaji wenyeji wa mkutano huo wa makanisa ya hapa Dar. upande wa matangazo kutakuwa na cinema za mikanda ya mwijilisti huyo itakayoonyweshwa kwenye nitaa mbalimbali ya hapa Dar.


Bonnke anakuja tz baada ya kupata mwaliko na askofu mkuu wa TAG ampaye alikutana naye mapema mwaka huu huko marekani, kwa mara ya mwisho mkutano wa mtumishi huyu ulifanyika mwaka 98 ambapo maelfu ya watu waliokoka na kufunguliwa. vipeperushi ambavyo vimeshatoka vinamtaka kila muumini aalike watu wasiopungua watu 10 ili waje kwenye huo mkutano. awali mkutano huo ulikuwa ufanyike katika viwanja vya jangwani lakini kutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea kwa sasa ilionekana itakuwa usumbufu kwa watakaokuwa wakitumia barabara ya morogoro.

 kama unataka kuwa mhudumu kwenye mkutano huo onana na mchungaji wa kanisa lako ili upewe maelekezo. ikumbukwe mwezi uliopita Bonnke alikuwa nchi ya Kenya na alifanya mkutano mkubwa sana katika viwanja vya uhuru na sasa ni zamu ya Tanzania na utafanyika viwanja vya nje ya uwanja wa uhuru.
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni