Jumanne, 16 Julai 2013

WANAWAKE WA DAR NA MWINJILISTI BONNKE KUTEMBELEA MAHOSPITALINI KAMA UNATAKA UWE MMOJAWAPO USIKOSE ALHAMISI HII

Alhamisi ya wiki hii (kesho kutwa) kutakuwa na kusanyiko la wamama na mabinti katika kanisa la Magomeni TAG, kuanzia saa 3 asubuhi, Cordinator wa mwinjilisti Bonnke atakutana na wanawake hao ili kupanga siku inayoitwa JESUS DAY. ambayo lengo lake kubwa itakuwa ni kuwatembelea wenye mahitaji katika mahospital mbalimbali katika jiji la Dar, katika siku hiyo na Bonnke mwenyewe atakuwepo katika huduma hiyo, vilevile kutakuwa na siku ya kuonana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwapo Rais J. Kikwete.


 hivyo wanawake na mabinti mnatakiwa kukusanyika kwa wingi ili kuja kupata hiyo semina ya namna ya kuanda hiyo JESUS DAY, namna ya kufika Magomeni TAG panda basi lolote linalopita Magomeni vituo vyakushuka ni Mikumi kwa mnaotumia barabara ya Kawawa na Kituo cha Usalama mnaotumia barabara ya Morogoro. nyuma ya kituo cha mikumi utaona kanisa kubwa la paa la kijani hapo ndipo inapofanyika semina. Usitamani kukosa.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni