Kwa miaka mitatu mfurulizo amekuwa akishiriki mashindano hayo na mwaka huu kaibuka kidedea |
Mwimbaji nyota wa gospel nchini mwanamama Christina Shusho ametwaa tuzo
ya mwimbaji wa mwaka kwa nchi za Afrika mashariki katika tuzo za Africa
Gospel Music Awards zilizofanyika usiku wa kuamkia leo jumapili katika
ukumbi wa The great hall chuo kikuu cha Queen Mary jijini London nchini
Uingereza.
Shusho amepata tuzo hiyo katika kinyang'anyiro cha waimbaji wapatao tisa
kutoka Kenya pamoja na Uganda huku Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na
waimbaji wawili, Shusho pamoja na Martha Mwaipaja ambapo hii ni mara ya
tatu kwa Shusho kuingizwa katika kinyang'anyiro hicho na hatimaye safari
hii kura zimetosha ameondoka na tuzo ambayo imepokelewa kwa niaba yake
na mkurugenzi wa GK Ambwene Mwamwaja.
Pamoja na Christina Shusho mwimbaji aliewika zaidi kwakuondoka na tuzo
mbili kati ya tatu alizopendekezwa ni mwanamama Ntokozo Mbambo wa
Nqubeko ambaye hata hivyo hakuhudhuria tuzo hizo ambazo zilikuwa na
kasoro za kiufundi za hapa na pale huku mwimbaji kutoka DRC mwenye
makazi yake nchini Uingereza bibie Dena Mwana aliweza kuwasimamisha watu
kwa uhodari wake katika uimbaji. Kiujumla waimbaji kutoka Afrika
magharibi, Ghana na Nigeria wameondoka na tuzo hizo zaidi ukilinganisha
na waimbaji kutoka sehemu nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni