WAUMINI WA KANISA LA AG IRAN |
Kanisa la The Central Assemblies of God Church la mjini Teheran limefungwa alhamisi ya wiki iliyopita tar 23-06-2013 na dola la nchi hiyo kwa kile kinachodaiwa ni kujaribu kuyabana makanisa nchini humo yasiwe na uhuru wa kuabudu, makanisa mengi katika nchi hiyo yana kumbwa na misukosuko kila mara ikiwa pamoja na kuwekwa vizuizini kwa wachungaji wa makanisa hayo. kabla ya tukio hilo halijatokea alikamatwa mchungaji mmoja Pastor Robert Asseriyan na akapelekwa kusiko julikana.
nchi ya irania ambayo iko chini ya utawala wa kiislamu imekuwa ikiwabana wananchi wake kuchagua dini ya kuabudu na kutakiwa kuabudu kwa dini ya kiislamu tu. ijapo kuna wageni wanaoishi katika nchi hizo ambao ni wakristo wamekuwa wakinyanyaswa sana na kama ikitokea mzawa akaokoka wakati mwingine huukumiwa jela maisha au hata kunyongwa na kuwa kitisho kwa watu wa nchi hiyo kuweza kuwa wakristo, pamoja na hayo bado ambao wanaendelea na harakati za kuhubiri injili ya Bwana Yesu na wana kumbana na vikwazo mbalimbali, mpendwa unaombwa kuendelea kuombea wakristo walioko katika nchi za kiislamu ili Mungu awatie nguvu na kuwaongeza. amina
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni