Jumanne, 11 Juni 2013

KAKOBE AWAAGA WASHIRIKA WAKE KWENDA KWENYE MKUTANO WA KIHISTORIA CANADA






 Hatimaye Askofu Zachary Kakobe amejitokeza katika ibada ya Jumapili hii na kuzungumza mengi kuhusiana na wito wake wa kuhubiri na kufundisha utakatifu Duniani, Askofu Kakobe alianz aibada hiyo ya mahubiri kwa kusema, mtu ukiwa na pesa unaweza kupata chochote cha hapa Duniani, lakini huwezi kupata vitu vya rohoni kwa njia ya pesa, vitu vya rohoni unaweza kuvipata kwa njia ya maombi pekee yake, aliyasema hayo Kakobe kwa kusoma maandiko ya kitabu cha Mathayo 6:33
Mungu wakati anampa ramani na agizo la kwenda kwangu kuhubiri Canada, tangu nipewa agizo hilo hadi leo, imekwisha pita miaka mitatu, wakati wote huo nipo kimya nautafuta uso wa Mungu nikimwomba anipe karama na vyote vinavyohitajika kwaajili ya wale walioko huko , wakati napewa maelekezo hayo nikama vile mtume Petro alivyokuwa anapewa maagizo ya kwenda kuvua samaki
Ibada hiyo iliambatana na shangwe na vigelegele vingi vya; haleluya haleluya amen amen na wengine kutokana na furaha iliyokuwepo, walipiga vigelegele vya Yesu Yesu Yesu
Kuna watu wanaeneza uongo eti kakobe katoroka, ndugu zangu nitoroke kwenda wapi, mimi sijatoroka, lakini nakwenda Canada kwaajili ya kulitimiliza agizo la Mungu alilonipa, nimekwisha imaliza kazi hapa Tanzania, nimekwisha kuhubiri vijiji karibia vyote hapa Tanzania, na nimehubiri kwa njia ya Tv kwa miaka mitano kwa gharama kubwa, fedha zilizotumika kulipia vipindi vya Tv kwa muda wote huo, ni zaidi ya shilingi bilioni tatu, nimekwenda Kenya, Zambia, Congo, Burundi nk kwahiyo nimefanya kazi na kwa hapa kwenda nikama kazi nimeimaliza, na sasa napaa kwenda Canada ambako ndio miisho ya Dunia
Wanangu Mungu ametuinua sana, ule uwanja nitakao utumia kule Canada ni uwanja wa kisasa sana ambao umezinduliwa miaka ya hivi karibuni, na sio uwanja unaoweza kutumiwa na mhubiri yeyote, lakini kwakuwa ni mpango wa Mungu, sisi Fgbf tunakwenda kuutumia na wazungu wataokoka kwa wingi wao. Katika mkutano huo Kakobe atakuwa akihibiri pamoja na wahubiri mbalimbali kutoka Marekani nan chi nyinginezo, pia mwimbaji mashuhuri Duniani Don Moen naye atakuwepo
Canada ni nchi tajiri sana na watu wenye kujivunia utajiri wao, na ndio maana, hata Rais wetu akienda kule huwa hapokelewi na mkuu wanchi ile, wanaompokea ni watu wa kawaida kama vile viongozi wa kitongoji furani, pamoja na yote waliyonayo, kakobe anakwenda kuwahubiri Injili na kuwangoza sala ya toba. Na kwa taarifa yenu nimekataa kuhubiri kwa kiingereza, safari hii nahubiri kwa Kiswahili kwa lengo la kujenga utamaduni wa kitanzania na kuiletea heshima Tanzania

Kwahiyo mkisikia mtu anasema Kakobe ametoroka, huyo mnapaswa kumpuuza kabisa kwasababu huyo anakuwa ni shetani, hata mimi ningekuwa shetani lazima ningezungumza maneno kama hayo, kwavile shetani anajua kinachokwenda kufanya kule
Wakati hayo yakienda kutendeka kule Canada, sauti ya kanisa imepata taarifa kwamba, Askofu Kakobe wiki mbili zilizopita alipatwa na msiba wa kuondokewa na mama yake mzazi, kifo na msiba huo, ulitokea huko Mkoani Kigoma, katika kijiji cha Kakonko, ambako ndio kwao na Kakobe, kwa taarifa ni kwamba Askofu Kakobe hakwenda kuaga wala kumzika mama yake mzazi, kutokana na majukumu aliyonayo kihuduma na maombi mazito kwaajili ya kuhubiri Injili Canada na Duniani kote.
Kwahakika Kakobe ni mtumishi aliyejitoa kipekee sana kutenda kile alichokiamini, sio raisi kwa mtu mwingine kuwa na viwango vya juu kiasi hiki ikiwa haujajitoa kama Kakobe, tunaamini kwamba atakuwa kielelezo kwa wengi na hasa kanisa lake na wachungaji wa kanisa lake, ya kwamba kama kuna jambo la kiroho basi ni muhimu walitangulize hilo kuliko kwenda kuzika wazazi wao!
Sauti ya kanisa, inamtakia safari njema Askofu Kakobe na kumtakia kila la heri huko Canada, kama alivyosema mwenyewe kwamba, anakwenda kuchukua medali ya dhahabu, basi sauti ya kanisa inamtakia heri, sio dhahabu moja bali ziwe nyingi

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: