Get information, challenges, News, Funny event, Gospel musician picture & profile documentary .and so more.
Jumapili, 5 Mei 2013
PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA NA MAELEZO YA MKUU WA POLISI MKOA WA ARUSHA. MWANAKWAYA 1 AFARIKI
RPC- ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU….WATU 3WANAHALI MBAYA, 1 AFARIKI NA 60 WAMEJERUHIWA
Mkuu wa Mkoa Mulongo naye amefika eneo la tukio na kuwafariji wahanga wa tukio la bomu….
RPC wa mkoa wa Arusha naye aliambatana na mkuu wa mkoa na muda huu alikuwa anatoa nasaha zake kwa wananchi….
RPC ameeleza kuwa tukio hili ni la kigaidi. Katika maelezo
yake, RPC amesema kuwa aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa
kujificha na kurusha bomu. …
Amesema Polisi wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa ni 60 .Hao wana majeraha ya kawaida na 3 wako mahututi na 1 amefariki. Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi
Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi umeimarishwa
Viongozi
wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla
ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa
Polisi.
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
Meya
wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa
miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi
kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi
kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote
waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa.
Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika
eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa
tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa
Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo
lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia.
Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa
vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa
Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni