Alhamisi, 2 Mei 2013

MKESHA MKUBWA UNAOKUTANISHA WATU WENGI AFLEWO. ZNZ, WATU DUNIANI KOTE KUUONA LIVE


AFLEWO ni nini?

·        AFLEWO ni kifupi cha “Africa Let’s Worship” ambayo maana yake ni Afrika Njoo Tuabudu

·        AFLEWO ni mradi wa uimbaji katika Afrika ambao ulianza mwaka 2004 nchini Kenya na baadae kuenea katika nchi ya Tanzania na Rwanda.

·        Tanzania huduma ya AFLEWO ilianza 2011 na mwaka huu 2013 ni Aflewo ya Tatu Kufanyika.

Nini maana ya maono ya AFLEWO?

KUTIA TUMAINI KATIKA YESU KUPITIA MATUKIO YA KUABUDU MARA MOJA KWA MWAKA KATIKA MUZIKI NA MAOMBI IFIKAPO MWAKA 2017.

Hapa Tanzania AFLEWO ilianza mwaka 2011 na mkesha wa kwanza ulifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 20/4/2011 na kuhudhuria na watu karibu ya 5000.

Mwaka 2012 tukio la AFLEWO lilifanyika kanisa la CCC, Upanga na kuhudhuriwa na watu karibu ya 5000.

Mwaka huu Mkesha Wa Aflewo Unafanyika Katika Ukumbi wa Kanisa la BCIC Mbezi, kuanzia saa 3:00 Usiku Mpaka saa 12 Alfajiri.

Aflewo Mwaka 2013 Imeboreka zaidi baada ya kuongeza miundombinu ya utendaji kazi kwa kutanua Uwigo wa Ushirikishwaji wa Makanisa Katika Kufikia Kilele Cha Aflewo Mwaka 2013.

Mikesha yote ya Aflewo inakuwa haina kiiingilio ni event ya bure kwa ajili ya Kila Mmoja.[1]


Nini Kusudi Kuu la Mipango Ya AFLEWO?

1.     Kuleta uzoefu wa kua “Mwili Mmoja”...ndio maana Aflewo si Mkesha wa Kanisa Moja.

2.     Kuombea Taifa La Tanzania hususani katika Amani, Uchumi, Upendo etc.
Kuombea Kanisa la Tanzania Kwa Ujumla TUKIO HILO LITAONEKANE DUNIA NZIMA KUPITIA MTANDAO WA INTERNET


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni