Jumanne, 5 Machi 2013

MHUBIRI WA KIMATAIFA BENNY HIN AFUNGA HARUSI MARA YA PILI KWA MKE YULEYULE. NI FUNDISHO GANI KWA WATUMISHI?

Siku ya jumapili ya tar 03/03/2013 ambayo ni kumbukumbu ya harusi ya blogger Martin ndiyo siku ambayo mhubiri wa kimataifa Benny Hin alifunga harusi nyingine mbele ya umati wa watu waliohudhulia ibada hiyo. bi harusi ambaye jina lake ni Suzane waliadhimisha siku hiyo ya muhimu sana katika familia yao huku watoto wake na wajukuu wakishuhudia.
Hapa wakila viapo vipya
ikumbukwe kuwa Benny na Suzan walitengana mwaka 2010 kutokana na sababu alizozitoa Suzani kuwa Mumewe Benny yuko busy na huduma kuliko familia na aliamua kuachana nae, kwa kipindi hicho Benny hakuwa na la kufanya bali kukubaliana na wazo hilo hivyo wakatengana. lakini mwaka jana ikatokea muujiza wa kurudiana na wakapanga siku ambayo wataihuisha ndoa yao mbele za umati wa watu na ndiyo ilikuwa jumapili ya tar 03/03/2013


ilikuwa ni siku ya furaha kwa wawili hao kurudiana tena kuishi kama mume na mke kama zamani ,

KUNA CHANGAMOTO GANI HAPA KWA WATUMISHI WA MUNGU
kuna kazi sana ya kugawanya muda kati ya familia na huduma kuna mchungaji mmoja alimuuliza mwanae akikua anataka kuwa nani akataja lakini haukuwa uchungaji, akamuuliza kwani we hutaki kuwa mchungaji kama mimi baba yako. mtoto alikata na kusema hiyo siyo kazi nzuri hupumziki hutuli nk. kuna wakati wa familia na kuna wakati wa huduma usipoweza kugawanya muda hapo ndo inatokea ya Ev Benny Hin.

 kuna mtumishi mwingine wa Korea Yong Choo yeye aliwahi kusimulia kisa ambacho ilibidi Mungu aingilie kati ili familia yake ipone. alieleza kipindi hicho alikuwa bado kijana na upako wa kuwahubiria wenye dhambi ulikuwa unachemka alichokuwa anafanya alikuwa na muda mwingi wa kusafiri kwenda kuhubiri akirudi safari hii anaagiza abadilishiwe nguo na kusafiri kwenda sehemu nyingine kuhubiri na akawa busy na kuhubiri. ikafika siku Mungu akasema naye akasema amsikilize mkewe anachotaka, baadaye alimuuliza mke wake akamwambia anataka watoke out kama wik hivi wakakae hotelini jambo hili lilimuumiza sana Yong aliwaza yani watu wana kufa dhambini mke wangu ananiambia twende tukastarehe, lakini kwa sababu Mungu alimwambia amsikilize mke wake ikabidi aende.


walivyofika huko ukawa na wakati wa kucheza kufurahi, mke wake akafika sehemu akaona kipepeo akaanza kumfukuza na kumfuata hapo yong Choo akaumia jamani sasa hii nini watu wana kufa dhambini yani ndo tunakuja kufukuza vipepeo hapo Mungu akasema naye kuwa amsaidie mke wake kufukuza kipepeo naye aka kimbia kuanza kufukuza kipepeo na mkewe.
Mwinjilisti Bonke ni moja kati waliohudumu katika  ibada hiyo 
hii inaonyesha kuwa japo kuna huduma lakini ni vyema kutenga muda wa familia ili na mke na watoto wapate  kuwa karibu na baba yao. tunawatakia maisha mema na ya utele.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 2 :

MOVEMENT FOR JESUS alisema ...

Ukiona vyema tuwekee na huo ushuhuda wa Choo.
Nimeupenda.

MOVEMENT FOR JESUS alisema ...

Hili ni tendo la Ushujaa sana.
Watumishi wengi hawako tayari kufanya matengenezo hasa wanapokosea hujihesabia haki kuliko toba.

Ni jambo la kupongeza sana.