Jumatatu, 4 Machi 2013

KANISA LA TAG LANUSULIKA KUCHOMWA HUKO KILINDI TANGA . PAMOJA NA UCHOMAJI WA MAKANISA UNAOENDELEA BADO MAKANISA MENGI YAENDELEA KUFUNGULIWA UKANDA WA PWANI YA TANZANIA

Kanisa la TAG huko Tanga kilindi limenusulika kuunguzwa na moto na watu wasiojulikana. akielezea tukio hilo mlinzi wa kanisa hilo alisema kuwa akiwa ndani ya kanisa majira ya saa 8 usiku alisikia watu wakitembea nje ya kanisa hilo na baada alipotoka nje aliona watu wanakimbia na kukuta walikuwa wameshamwaga mafuta ya petrol tayari kwa kuwasha moto hivyo zoezi hilo likawa limeishia hapo.

wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa mkoa wa Tanga wamewataka wana Tanga kudumisha amani na utulivu na kuachana na mambo ya vurugu za kidini ambazo zinaweza ipeleka nchi mahali pabaya. hata hivyo pamoja na uchomwaji wa makanisa unaoendelea kumekuwa na ongezeko la makanisa mapya yanayofunguliwa katika ukanda wa pwani ya Tanzania, maeneo hayo ni Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es salaam, Tanga na Zanzibar. uchunguzi mdogo ulifanya na blog hii katika mkoa huu wa Dar es Salaam umaonyesha makanisa mengi sasa yamefanyiwa na mengine yanaendelea kufanyiwa ukarabati wa upanuzi wa makanisa yao na makanisa mengine yameongeza idadi ya ibada baada ya watu kutokutosha katika ibada moja. vile vile kuna makanisa mengi yanaendelea kufunguliwa.

wiki mbili zilizopita blogger wa blog hii ameweza kuwaelekeza wachungaji wa 3 ambao wote wanafungua na wengine wameshaanza huduma katikati ya mji wa Dar, aidha mpango mkakati wa kanisa la TAG umekuwa chachu kubwa ambao umewezesha kufungua vyuo vya mafunzo ya muda mfupi (vyuo vya kupanda makanisa) ambao waliomaliza wengi wamefungua makanisa yao, mkoani Lindi kuna chuo kimefunguliwa pale Mtamaa na kuwa kichocheo kikubwa cha kazi ya Mungu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na hata katika visiwa vinavyozunguka maeneo hayo.

Najua kuna upepo unaopita lakini kuna dalili za uamsho mkubwa ambo uko mbele baada ya huu upepo wa uchomwaji wa makanisa kupita maana kila lenye mwanzo lina mwisho na ninaamini Mungu wetu hatakaa kimya lazima awatete watoto wake wanao mwomba yeye kila wakati hata wale waliotangulia katika Bwana najua watapata thawabu zao.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni