Jumatatu, 4 Machi 2013

MAZNAT BRADAL IMEANDA SHEREHE KUBWA YA KUAZIMISHA MIAKA 10 TANGU KUANZISHWA. USIKOSE KUISHUHUDIA DIAMOND JUBILEE 05/05/2013

Kwa watu ambao wamekuwa wakijihusisha na issue mbalimbali za Mambo Ya Harusi na Mapambo ya Harusi Jina la Maznat si geni sana sana kwa Wakazi hasa wa Jiji la Dar-es-Salaam. Ule Msemo Wa Start with Nothing Finish With Everything umedhihirika kwa safari iliyoanza mwaka 2003 kwa MAZNAT kuanza kutengeneza Maharusi mpaka sasa ambapo Maznat ni Kampuni Kubwa ya Kuwandaa Maharusi Wadini Zote na Hata Wale Wasio na dini yoyote.


Akielezea namna alivyoanza mradi huo alisema kuwa mwanzo alianza kwa kuwafuata maharusi majumbani kwao baada ya kuona kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo na baadae Mungu akamsaidia na kujenga chumba kimoja na kuanza kazi ya kuwapambia kwenye hiyo saloon yake ndogo, alianza na mtaji mdogo lakini Mungu alimsaidia kuukuza huo mtaji wake kutoka chini na kuendelea kuongezeka kidogo kidogo mpaka akaanza kuajiri wafanyakazi  kwa ajili ya kusaidia kwa sasa ameweza kufikia mafanikio makubwa ijapo bado hajafika pale anapotaka yeye. eneo ilipo unaweza kupata mahitaji yote ya mapambo ya bibi harusi yaani shela, heleni, mikufu, mataji, maua harisia ya mikononi, vipodozi original, nywele mitindo yote na unapata ushauri katika maswala upambaji. MAZNAT watatoa maelezo ya Kutosha Siku hiyo namna ya Kuondoa Stress Unapokuwa ukijiandaa kwa habari ya Harusi ama Send Off au Kitchen Part.

                               
aliendela kuelezea mambo mbalimbali ya mbeleni ana mpango wa kufungua MAZNAT BRIDAL ONE STOP ambapo mtu atapata mahitaji yoote ya kupamba maharusi yaani bibi na bwana harusi, chuo kitakacho wafundisha watu wanaotamani kufanya kazi hizo, sehemu ya kufanya maombezi na ushauri katika maswala ya ndoa, vile vile kuna MAZNAT BRIDAL MAGAZINE ambayo itazinduliwa siku hiyo ya tarehe 05/05/2013
Mmiliki wa salooni hiyo ambaye ni msomi na mambo yote yayoendeshwa kisomi aliendelea kusema huko baadae atatoa huduma ya kutengeneza makeup waigizaji wafilamu maana anauwezo wa kumfanyia mtu makeup akaonekana ameungua au anakidonda nk. hivyo katika kumshukuru mungu ndiyo ameandaa hiyo siku kwaajili wa kuwakutanisha wanawake wajasilia wanaohusika katika suala zima ya harusi wakiwamo washonaji wa nguo wapika vyakula n.k
Zawadi Mbalimbali Zitatolewa Siku Hiyo ambapo Magauni Ya Harusi yenye Thamani ya Shilingi laki 9 kushindaniwa, Gharama za Kutengenezwa Bibi Harusi Kufidiwa siku ya Shughuli Iwapo Mtu atashiriki katika Mchakato Huo, Namna ya Kushiriki Nunua Tiketi Yako MAZNAT eneo la Mikocheni Pale Bajaj za Mikocheni B zinapoishia Kisha Utapewa Masharti Nafuu kabisa za Kujishindia Shela La Harusi na Mapambo ya Bi harusi na Matron wake.
Usikose Siku hii tarehe  5 May, 2013 kuanzis saa 9 alasiri ambapo utaweza Kumsikiliza Mfanyabiashara Mwanamke aliyeokoka akieleza Changamoto mbalimbali za tangu alipoanza kupamba watu majumbani kwao mwaka 2003 mpaka sasa anapofikiria kuwa na Shopping Centre ya Mambo ya Harusi siku hiyo. Yote Yawezekana Kwake aaminiye
MAHALI: JIAMOND JUBILEE
SIKU: 5 MAY 2013
MTUPIO: KITENGE CHA KANTE( kinapatikana Mazant Bridal Mikocheni)
WAIMBAJI WATAKAOKUWEPO: Bahati Bukuku, The Voice na wengine.
Kwa mawasiliano: 0752 666670, 0783 444470, 0718 818999
 
Zawadi itatolewa kwa bibi harusi aliye na watoto watatu na bado akaweza kuvaa gauni lake la harusi.
Gauni 3 za harusi zitatolewa kwa bibi harusi watarajiwa kama zawadi.
Christian Bloggers tulipata nafasi ya kupata breakfast pamoja nae naye alikua na haya ya kusema:
 
Bloggers: Ulianzaje Maznat hadi imefika hapa ilipo?
Maznat: Tulianza nyumbani na wakati mwingine nlikua nafanya bure, baadae tukaahamia kwenye chumba kimoja, na nlikua nawapamba na kuwatengeneza marafiki zangu na waumini wenzangu kanisani. 

Bloggers:Nini siri ya mafanikio yako?
Mazant: Kwa kweli nakiri kuwa ni Yesu tu ndie aliyeniwezesha kufika hapa nilipo leo. Lakini pia consistance and courage. Sikuwai kuacha kufanya kazi hata kama sikupata faida siku hiyo, niliendelea tu. my motto always is; "if you can dream it you can have it".

Bloggers: Mafanikio gani ambayo umeyapata?
Maznat: Mafanikio yako mengi sana, namshukuru Mungu kwa hilo. Kwanza nimeweza kujenga mahusiano na watu, nimefahamiana na watu wengi, nimetengeneza ajira kwa watu wengi, nimebadilisha pia mtazamo uliokuwepo juu ya beauty industry.

Bloggers: Kila penye mafanikio kuna changamoto. Ni changamoto gani umekutana nazo katika safari hii ya miaka 10 na Maznat?
Maznat:Bidhaa feki, ni changamoto kubwa sana ambayo tunakutana nayo, na ili kupata bidhaa original nna lazimika kusafiri mwenyewe kwenda kuzileta. Pili, wateja wanakua hawapo tayari kulipia huduma nzuri na bidhaa original. Utamhudumia mtu vizuri, alafu ikifika saa ya kulipa inakua usumbufu, na umetumia product original.

Bloggers: Saluni nyingi wana kawaida ya kubadilisha wafanyakazi, vipi wewe?
Maznat: Mimi kwa kweli nakaa sana na wafanyakazi wangu, siri kubwa ni kuwajali. Mimi nimewafungulia saccos, nawalipa vizuri kwa hiyo mtu hawezi kuondoa mahali ambapo anauhakika na maisha yake.

Bloggers: Umewahi kusomea au kwenda shule ya beauty?
Maznat:Ndio. nimesomea, nna diploma ya beauty, lakini pia mimi ni Mwanasheria by Proffession, nina Masters ya Sheria, na pia nimesoma Certificate ya Human Resource ambayo pia imenisaidia kujua namna ya kuongoza wafanyakazi wangu. Napenda tu kusema, Biashara ukiwa umesoma ni rahisi zaidi ukilinganisha na mtu anayefanya biashara akiwa hajasoma.

Bloggers: Tuambie kuhusu hii miaka 10 ya Mazanta Bridal.
Maznat: Kwanza ni siku ya kumshukuru Mungu kwa Maznat Bridal kufikisha miaka 10, tangu mwaka 2003 hadi leo sio safari ndogo. Siku hito tunatarajia takribani wanawake 800, wakiwepo ma bibi harusi waliowahi kupambwa na Maznat, ma bibi harusi watarajiwa, wateja wooote wa Maznat, wajasiliamali wanawake na wanawake woote wa jiji la Dar. Wajasiliamali watasikia jinsi Maznat ilivyoanza hadi hapa ilipofikia.

Bloggers:Je, kuna kiingilio?
Maznat:Kiingilio ni elf 50,000/= tu, pamoja na kitenge cha sare aina ya kante.

Bloggers: Itaanza saa ngapi?
Maznat: Itaanza saa tisa mchana hadi saa tatu usiku.

Bloggers:  Unawezaje kubalance familia na kazi?
Maznat: Kwa kweli namshukuru Mungu familia yangu inanipa full support, nina mume very inteligent and very supportive. Napata full support kutoka kwenye familia yangu.

Bloggers: Una neno gani la mwisho la kuwaambia wasomaji?
Maznat: Nawaambia waje hiyo tarehe 5 May 2013,pale Diamond Jubilee, kutakua na mambo mengi sana mazuri. Wajasiliamali wanawake waje wasikie ushuhuda wa Maznat ilipotoka hadi hapa ilipo.Nawakaribisha wote. 

Bloggers: Asante sana.
Maznat: Asante sana.
Hii ni Sehemu Ya Duka La MAZNAT ambapo kuna mahitaji Ya Wanawake Kwa Urembo na Harusi pia.Baadhi Ya Christian Bloggers Wali attend MAZNAT-Bloggers Breakfast                      
Hii kitu ilimchanganya Papaa ambaye mwaka huu anampango wa kuoa

                                
 Yamejaa Kibaoooo haya magauni Meupe a.k.a Shela


Christina Bloggers Wakienda Sawa

Mamaa MAZNAT akitoa Ufafanuzi Juu Ya Sherehe Ya Kutimiza Miaka 10.

Jamani Karibu Chai Sasa baada ya Kazi...


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni