Ijumaa, 1 Machi 2013

AFLEWO TANZANIA 2013 BISHOP BREAKFAST YAFANA SANAKatika Kuelekea Event ya Aflewo Tanzania 2013,Siku ya jana ilikuwa Bishops Breakfast Forum katika Hotel ya Regency Park Mikocheni, ikiwa ni katika kuwashirikisha Maaskofu na Mtume wa huduma mbalimbali maono na maana ya kuwepo kwa Aflewo Tanzania mwaka 2013.

Mnamo terehe 5-5-2013 BCIC Mbezi Beach itakuwa ni usiku wa aina yake katika Kumsifu na Kumuabudu Mungu ambapo Aflewo Mass Choir yenye waimbaji zaidi ya 90 watapaza sauti zao wakiimba sifa kwa Mungu.

Katika Bishops Breakfast hiyo iliyoudhuliwa na baadhi ya Maaskofu kama
Apostle Ntepa,Bishop Fredie Kyara, Bishop Elly Mwende,Bishop Simtovu,Bishop Mwasota, Bishop Shegga, Pastor Fredie (UpperRoom Minisry )Bishop Gamanywa alitoa hudhuru kwa Kuwalilishwa na Pastor Amoni Kalahilo na wengine wengi na kusifu Aflewo kuweza kuwa kutanisha na wao kama Maaskofu katika Jiji la Dar es salaam kuwashirikisha Maono ya Aflweo Tanzania na kusifu juhudi zinafanywa maana ni katika Kuujenga mwili wa Kristo na kulileta pamoja Kanisa la Tanzania na Afrika Kwa Ujumla.
Kikao cha watumishi wa Mungu

Pastor Paul Safari na Abel Orgenes Kama walezi wa huduma ya Aflewo Tanzania, wakieleza umuhimu wa huduma hiyo kwa waimbaji ni pamoja na kukua kwa maisha ya kiroho kati ya waimbaji na Mungu maana tofauti na uimbaji pia kuna mafundisho kuhusu Maisha ya wokovu na Maana ya Kufisu na Kuabudu kwa ujumla
Pastor Safari akifafanua jambo

Pastor Abel akiongea

Pastor Fredie Kyara aliweza kutoa ushuhuda wa jinsi Mkesha huo ulivyo wa baraka sana kwa kusema jinsi ilivyoweza kukutana na uwepo wa Mungu kwa Mkesha uliopita mwaka 2012,na kusihi Maaskofu wengine kukubali na kuunga mkono huduma hii ya Aflewo kwa kuwa ruhusu waumini wao makanisani kuhusika kikamilifu.
Pastor Kyala akiongea

Kwa kumalizia Maaskofu hao walipata nafasi ya kuchangia na kusema kuwa wanakubaliana kwa nia moja na kusema wako tayari kushiriki kwa namna moja au nyingine kuhakikisha mkesha wa Aflewo Tanzania 2013 unafanikiwa."
Watumishi wakibadilishana mawazo


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni