Alhamisi, 10 Januari 2013

FLORA MBASHA MWIMBAJI ANAYE PASUA ANGA LA KIMATAIFA DUNIA ITAMWONA KWA MARA NYINGINE

Katika miaka ya hivi karibuni mziki ya injili umekuwa ukipiga hatua kubwa kwenda kimataifa baada ya waimbaji wengi wa mziki huo kupata mialiko kwenye nchi mbalimbali Duniani. hii inaonyesha kuwa mziki huo unakubalika sana na kupendwa na watu wengi na kingine kuwa na upako kutokana na anayeimbiwa katika nyimbo hizo ni Mungu mwenyewe.
Mbasha Akiwa na Salim Kikeke nyuma ni Charles Hilary
 
mwaka jana tumeona waimbaji mbalimbali kama Upendo Nkone, Upendo Kilahilo, Christina Shusho, Rose Mhando na Flora Mbasha wakiwea pipa na kwenda nje ya bara la Afrika kufanya huduma ya uimbaji na ambayo imekuwa na manufaa makubwa sana kwa waimbaji wenyewe lakini hata kwa mziki wa injili nchini.

Mbasha akihojiwa Radioni na John Solombi
 leo nataka nimuongelee Flora Mbasha ambaye yuko katika ziara yake UK na baadae ataenda Australia. katika ziara yake ametembelea BBC ambalo ni shirika kubwa la habari duniani ambalo habari zake zinasambazwa duniami kote. kufanyika kwa mahojiano hayo yanaendelea kufungua ukrasa mpya katika tasnia ya nyimbo za injili. hii ni mara ya pili kwa flora kuhojiwa na kituo kikubwa cha habari baada ya mwaka jana kuhojiwa na VOA (Voice of America) alipotembelea huko. kwasasa ninaweza kusema kuwa amebakisha kituo kimoja ambacho nacho ni kikubwa duniani yaani DW sauti ya Ujerumani na namwombea siku ifike nako afike kama imewezekana VOA na BBC hata DW inawezekana.

Mbasha akihojiwa kwenye TV na Salim Kikeke

katika mahojiano mafupi sana niliyofanya nae amehojiwa na radio pamoja na TV ambavyo kuna uwezekano vipindi hivyo vya mahojiano kuonyeshwa na kusikika wiki hihi. amesema baada ya kumaliza ziara yake UK wataelekea Australia ambako huko nako watafanya huduma huko.

Mbasha akiwa na watangazaji wa BBC swahili Salimu Kikeke na John Solombi

Mbasha na John solombi

Baada ya kukausha koo kwa mahojiano hapa anaburudisha koo kwa vitu laini

Mbasha Akikata kiu

Mbasha akiwa na Charles Hiraly

Maandalizi ya Uso kabla ya mahojiano ya TV

Hii picha alipotembelea Sauti ya America Mwaka jana

blog hii inamwombea ahudumu salama huko aliko na jina la Bwana lijulikane duniani kote. Mungu ibariki Tanzania na bariki waimbaji woooote wa gospel

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni