Alhamisi, 10 Januari 2013

MCHUNGAJI YOUCER NADARKHANI ACHIWA HURU BAADA YA KUWEKWA KIZUIZINI WAKATI WA SIKUKUU ZA CHRISTMASWiki hii mchungaji wa Irani Youcef Nadarkhani aliachiwa kutoka kizuizini baada ya kuwekwa kizuizini katika msimu wa sikukuu ya Christmas.

Mke wake ni mmoja ya watu waliokuwepo siku alipoachiliwa huru katika gereza la Lakan lililoko kaskazini mwa mji wa Rasht alisema Firouz Khandjani ambaye yeye ni msirika wa kanisa la mchngaji huyo.
Ikumbukwe kuwa mchungaji huyo aliwekwa kizuizini zaidi ya miaka mitatu na kuachiwa mwaka jana na sikukuu hiyo ya Christmas ilikuwa ndo sikukuu yake ya kwanza kuwa na familia yake lakini wakamweka kizuizini.

.Mchungaji huyo ambaye anamtumikia Mungu katika nchi ngumu inayopinga kitu kinachoitwa ukristo amekuwa akipata misukosuko mara kwa mara na hata wakati mwingine walitaka kunyonga lakini Mungu mkubwa akamtetea, inakadiliwa kuwa Irani ina wakristo wasiopungua 100,000.
Nchi hiyo inaruhusu makanisa ya nyumbani tu na wasiwe wazawa wawe ni wahamiaji ambao wamekuja kufanya kazi nchini humu. Akitokea mzawa basi hatua kali huchukuliwa kutokana na nchi hiyo kuongozwa kwa mfumo wa Kiislamu.

Pamoja na kuwa ni nchi ya kiislamu kumekuwa na ongezeko kubwa la wa irani kubadili dini na kuwa wakristo na hilo ndilo linalosababisha nchi kuchukua hatua kali ya yeyote anayekutwa na hatia ya kubadili dini, pamoja ni hivyo mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu mara kwa mara zimekuwa zikiilaani sheria hizo za ukandamizaji wa haki za raia kuchagua aabudu dini gani.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni