Mtumishi
wa Mungu na kiongozi wa huduma ya Ngurumo ya Upako mtumishi Mhe Nabii Geordavie
mwenye makazi yake jijini Arusha,amekuwa ni mtumishi wa Kwanza nchini kumiliki
usafiri wa anga kwa ajili ya kufanyia huduma.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha
habari mtumishi huyo anamiliki HELKOPTA na tayari anazo documents zote za
umilikaji wa usafiri huo.
Hii
ndiyo Helkopta ya ya mtumishi wa Mungu Geordavie
|
Nabii
GeorDavie kwa sasa wengine wanamuita MAESTRO licha ya kumiliki usafiri huo wa anga
pia anamiliki kituo cha redio jijini Arusha kinachojulikana kama Ngurumo Fm
Radio.Mwaka huu wa 2012 umekuwa wa baraka sana kwa mtumishi huyo ambapo siku za
hivi karibuni alihitimu masomo ya THEOLOJIA kutoka chuo kimoja cha nje na
kutunukiwa PHD ya Theolojia.
Nabii
Geordavie Maestro akiwa ndani ya Ngurumo ya Upako Redio
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni