Jumatano, 3 Oktoba 2012

MGANGA WA KIENYEJI AOKOKA TANGA TUNGULI ZACHOMWA HADHALANI. NI ZA HASSANI

 Wengi tunajua kuwa mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa inayosifika kwa uchawi, pamoja na hivyo bado injili inahubiriwa na watu kumpa Yesu maisha yao. wiki iliyopita katika mkutano wa injili ulifanyika Lushoto mganga mmoja aliamua kuachana na tunguli zake na kumpa maisha yake mwanaume wa wanaume Yesu kristo. tukio lililowashangaza watu wanao mfahamu la kuamua kuleta tunguli zake na kuchomwa moto!!! ni sawa sawa na mtaji wako wa biashara kuupoteza lakini ndivyo alivyofanya bwa Hassani.
Bwana Hassani akikabidhi maisha yake kwa Yesu

Mzigo wa matunguli ukiwa umesambazwa chini

Tunguli zikichomwa moto mbele ya umati wa watu

Bwana Hassani akiwa ameshika tunguli zake

Mwinjilisti Msoloka akionyesha baadhi ya Tunguli


Mchawi huyo alikabidhi mzigo wa matunguli katika mkutano uliofanyika Lushoto mkoa wa Tanga ambao ulikuwa unahubiriwa na Mtumishi wa Mungu mwinjilisti Msoloka. mkutano huo uliandaliwa na EAGT kwa mchungaji Shetui ulikuwa ni wa siku tano. baada ya nguvu ya Mungu kufunika lushoto siku iliyofuata mchawi huyo alikuja na furushi lake la tunguli na kumpa Yesu maisha yake na siku iliyofuata alimleta na mke wake kuja kuokoka. Lushoto ambako karibu asilimia ni waislamu bado watu wapatao 150 waliokoka katika mkutano huo.
Lungu la Yesu akiimba kwenye mkutano huo

Hassani pamoja na Rungu la Yesu

pamoja na waimbaji mbalimbali waliokuwepo kuimba pia alikuwapo mwana hiphop kutoka Dar yaani Lungu la Yesu ambaye aliongoza mashambulizi kwenye uimbaji.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni