Alhamisi, 4 Oktoba 2012

VHM YAFANYA HUDUMA ZA KIJAMII YA KUGUSA NI KUONYESHA UPENDO WA MUNGU

Huduma ya VHM kipindi hiki imekuja kivingine katika kuwahudumia watu. VHM wamekuwa wakifanya huduma za kuwaleta watu kwa Yesu, kusaidia makanisa ya vijijini na kupeleka injili kule ambako bado hakujafikiwa na wahubiri. kote huko wamekuwa wakifundisha upendo wa Yesu kwa vitendo. kipindi hili wamekuja kuhudumia watu kwa upande wa afya zao. habari zilizoifikia blog hii zinasema kuwa kuna timu ya madaktali waliokuja kutoka marekani kwaajili ya kutoa huduma hiyo. pamoja na huduma hiyo ya kiaya bado watu wanafundishwa juu ya upendo.
Vipimo na Matibabu yakiendelea

watu wengi waliojitokeza katika huduma hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo jamii ina uhitaji mkubwa wa huduma za matibabu huku hospitali nyingi za serikali zikitoa huduma mbovu na kutokuwepo kwa madawa.huduma hii ambayo inatolewa bule kabisa ni kupima pamoja na kupewa dawa bure kabisa.
huduma hii imewanufaisha wakazi wa Kiwangwa na Kimanzichana vijijini
  • Walengwa ni watu wote wenye uhitaji wa kupimwa afya zao na kupatiwa matibabu
  • Ni zoezi la siku 2 kila kituo
  • Oct 1 -2 Kiwangwa
  • Oct 3 and 4 Kimanzichana
Mkurugezi wa VHM Mch Mitimingi akiongea na muhitaji





ni kweli injili inatakiwa kuhubiriwa kwa kila njia ili mladi kila mtu aweze kusikia habari njema za upendo wa Mungu ninajua kama wangeenda na spika zao wakatangaza kuna mkutano wa injili wasingejaa namna hii lakini kwa njia hii ya matibabu wamekuja watu wengi sana kama unavyoona kwenye picha na ukizingatia maeneo haya wengi ni waislamu. iende mbele injili hiyo- - - - - 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: