Jumatatu, 3 Septemba 2012

ST ANDREW YOUTH CHOIR YA ANGLICAN MAGOMENI YAFANYA ZIARA YA KUFANA SANA UGANDA


St Andrew Youth choir ya Magomeni Anglican ilifanya ziara katika nchi ya Uganda. habari zilizoifikia blog hii kuwa kulikuwa na tamasha lililokutanisha kwaya mbalimbali. Tamasha hilo lilikuwa ni zuri na la kufana sana. kwaya hii inayotumia uimbaji aina ya nota ilishiriki katika tamasha hilo ambalo uimbaji wake ulikuwa ni wa nota. kwaya hiyo inayoongozwa na mwl Steven Homanga ilifanya vizuri katika tamasha hilo na kulikuwa na nyimbo ambazo kila kwaya ilipangiwa kuimba na kulikuwa na wimbo wa pamoja, pamoja na hayo walipewa vyeti vya ushiriki wa hilo tamasha ambavyo wamegawiwa kila mwanakwaya.


Mwl wa kwaya Steven akitoa maelekezo ya uimbaji


Kwaya nyingi zikiimba wimbo wa pamoja

Kwaya ya Anglican Magomeni wakiimba huko Uganda

Waimbaji wa Akapela wakiimba

wimbo wa pamoja

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni