Jumamosi, 8 Septemba 2012

MSICHANA WA KIKRISTO ALIYEKUFURU, ACHIWA PASKISTAN

Jaji nchini Pakistan amemwachilia kwa dhamana msichana mmoja wa kikristo aliyekuwa ameshtakiwa kwa kosa la kukufuru dini ya kiisilamu.
 
Msichana huyo, Rimsha Masih, amekuwa akizuiliwa kwa wiki tatu kufuatia madai kuwa alichoma kurasa za Koran.

Tangu kukamatwa kwake, Masih, mhubiri aliyemshtaki, Khalid Chishti, pia alizuiliwa baada ya kudaiwa kuwa naye alikufuru dini.

Walioshuhudia tukio hilo waliambia wendesha mashtaka kuwa walimwona mhubiri huyo akiweka kurasa za Koran ndani ya mkoba wa msichana huyo.

Kesi hiyo imezua hisia kali miongoni mwa umma baadhi wakisema kuwa Pakistan inatumia vibaya sheria za kukufuru.
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni