Jumatano, 29 Agosti 2012

VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUOMBEA MCHAKATO MPYA WA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

MAKAMU Mwenyekiti wa Tume ya kukusanya maoni juu ya katiba mpya, Jaji Agustino Ramadhan, amewataka viongozi wa dini nchini kuombea mchakato huo ili kunusuru mkanganyiko utakaoweza kujitokeza baadaye.


Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi kwenye uzinduzi wa miaka 50 ya Chama cha Kujisomea Biblia Tanzania, alikiri mchakato huo kukumbwa na misukosuko mbalimbali.

“Ndani ya katiba, kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kuandaliwa kwa ajili ya miaka 50 ijayo, hivyo siwezi kufafanua zaidi ila kikubwa Watanzania, viongozi wa dini tunaomba muiombee ili kudumisha amani ya nchi yetu,” alisema Jaji Ramadhani.

Mbali ya hilo, alizungumzia pia suala la muungano kuwa unaweza kuwepo au la, na kama utakuwepo uandaliwe kwa namna gani.

“Suala la muungano inategemea, kwa sababu linaweza kuwepo au kutokuwepo, na kama likiwepo uwe wa namna gani, hiyo yote ni kujipanga,” alifafanua.

Jaji Ramadhani alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya Jumuiya ya Mihadhara ya Dini ya Kiislamu (Uamsho) ya Zanzibar inayopinga muungano, hakuweza kuzungumza lolote.

Naye Katibu Mkuu wa chama hicho Mchungaji Emmaus Mwamakula, alifafanua kuwa maadhimisho ya uzinduzi huo yatafanyika mkoani Mbeya Septemba 14.

Alisema kuwa, umoja wa kujisomea Biblia nchini umekuwa chachu katika jamii, hasa kwa kuwahudumia wanafunzi mashuleni na kutoa semina kwa vijana juu ya maisha
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni