Alhamisi, 30 Agosti 2012

ASKOFU DESMOND TUTU ASUSIA MKUTANO KWA SABABU YA TONY BLAIR

 


Desmond Tutu
Askofu mkuu Desmond Tutu amesusia warsha moja baada ya kukataa kushiriki warsha hiyo pamoja na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.
 
Tutu ambaye ni mwanaharakati mkongwe wa amani, alisema kuwa hatua ya Blair kuunga mkono vita vya Iraq, haikubaliki kimaadili, na kuwa hapaswi kuwa na ushirikiano wowote na yeye.
Wawili hao walistahili kushiriki katika warsha ya siku moja kuhusu uongozi mjini Johannesburg, Afrika Kusini hapo kesho.
Waakilishi wa Blair walielezea masikitiko yao kwa hatua ya askofu kuamua kujioandoa kwenye mkutano wao.

Tutu, aliyepata tuzo la amani la Nobel mwaka 1984 kwa sababu ya kampeini yake ya amani wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini alistahili kushirki mkutano kuhusu uongozi pamoja na bwana Blair.
                                                              Majeshi ya Marekani Iraq
 
Washiriki wengine ni pamoja na bingwa wa mchezo wa chess duniani ambaye pia ni mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi, Garry Kasparov pamoja na afisaa mkuu mtendaji wa maduka ya Tesco Uingereza Sir Terry Leahy.

Katika taarifa iliyotolewa kutoka kwa ofisi ya bwana Tutu, " Askfo Tutu anaonelea kuwa hatua ya Blair kuunga mkono uvamizi wa Marekani nchini Iraq,kwa misingi hafifu na madai ambayo hayakuwahi kuthibitishwa sio jambo linalokubalika kimaadili.

"Kauli mbiu ya warsha hiyo ya uongozi ni maadili na uongozi. Na kwa muktadha huu, itakuwa si vizuri kwa Askofu mkuu kushiriki na Tony Blair kwenye warsha hiyo.'' ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo taarifa kutoka ofisi ya Blair iliyotolewa kujibu hatua ya Askofu, ilisema kuwa wawili wao hawakupangiwa kushiriki pamoja.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa '' kuhusu swala la Iraq, wawili hao daima hawajawahi kukubaliana kuhusu kung'olewa mamlakani kwa Saddam hussein kwa nguvu , tofauti kama hizi ni nzuri katika mazingira ya demokrasia''

''Na ikiwa ni swala la maadili, hivi maajuzi kumeadhimishwa mauaji ya halaiki ya Halabja ambako maelfu ya watu waliuawa kwa siku moja kwa kumutumia silaha za sumu na kwamba kuhusu vita kati ya Iran na Iraq takriban watu milioni moja walifariki ikiwemo wale waliouawa kwa kemikali hizo za sumu. Kwa hivyo maamuzi haya daima hayawezi kuwa rahisi ukizingatia maadili na siasa.'' iliongeza taarifa hiyo.

Hatua ya Tutu kujiondoa kwa warsha hiyo inajiri huku chama kimoja cha kiisilamu nchini Afrika Kusini kikitangaza kupanga maandamano kupinga uwepo wa Balir kwenye warsha hiyo kwa sababu aliunga mkono vita vya Iraq.
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: