Jumanne, 28 Agosti 2012

BAADA YA KUUWAWA KWA KIONGOZI WA WAISLAMU MOMBASA SI SHWARI MAKANISA MAWILI YAVAMIWA

Watu 12 wamekamatwa na polisi kufuatia makabiliano kati ya polisi na vijana wanaofanya vurugu kufuatia kuuwawa kwa kiongozi wa kidini Sheikh Aboud Rogo siku ya jumatatu.
Baadhi ya mitaa ya mombasa kukiwa na vurugu

Katika siku ya pili ya vurugu hizo, wengi ya vijana hao wamekamatwa nje ya Msikiti Musa iliyo eneo la Majengo visiwani Mombasa.

Wakati wa makabiliano hayo polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na ghadhabu.

Hata hivyo katika eneo moja polisi walilazimika kutumia risasi za mpira kuwatawanya vijana waliokuwa wakiwasha matairi barabarini na kufanya uporaji.

Bwana mmoja alichomwa kisu katika karakana yake na kulazimika kupewa huduma ya kwanza na wafuasi wa dhehebu la Jeshi la wokovu.

Aidha imesemekana watu wamevamia makanisa mawili na kufanya uharibifu mkubwa ikiwapo kuchoma baadhi ya vitu vya makanisa hayo.

Na wakati Mombasa ikiwaka moto, wapiganaji wa Al shabaab wametuma ujumbe katika mtandao wao wakiwasihi waislamu wa kenya "wachukuwe kila hatua zinazostahili kulinda dini yao"

" Waislamu lazima wachukue sheria mikononi mwao, na wasimame kidete dhidi ya makafiri na kuchukua kila hatua kuilinda dini yao, heshima yao ,mali yao na maisha yao kutoka kwa maadui wa waislamu" , Al shabaab wamenukuliwa wakisema hayo katika taarifa yao.

Kiongozi huyo wa kidini Sheikh Aboud Rogo ,aliyepigwa risasi na kuuwa siku ya jumatatu alikuwa ametajwa na Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa kama mtua anayewasajili baadhi ya vijana wa Kenya wkenda kujiunga na wapiganaji wa Al Shabaab.

Sheikh Aboud Rogo pia anadaiwa kuwa alikuwa mfadhili wa kundi hilo la Al shabaab.

Mgogoro wa kidini waibuka

Waandamanaji walivamia magari na majengo mjini MombasaWaandamanaji walivamia magari na majengo mjini Mombasa
Waandamanaji mjini Mombasa walivamia makanisa mawili na kujaribu kuyachoma moto. Samani zilishika moto na baadaye moto huo uliweza kuzimwa kabla ya makanisa hayo kuungua kabisa. Makanisa yasiyopungua manne yalivamiwa na viti vilivyokuwa ndani kuvunjwa.

Kwa muda mrefu, uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu nchini Kenya umekuwa mzuri. Mkuu wa polisi wa mjini Mombasa, Kipkemboi Rop, ameeleza kwamba vijana walioshambulia makanisa walifanya hivyo kama jambo la ghafla na bila kufikiria. Naye Sheikh Juma Ngao, ambaye ni kiongozi wa kidini, amesema: "Vijana waliovamia makanisa labda walidhani kwamba aliyemuuwa Rogo lazima alikuwa mtu ambaye si Muislamu. Kwao, watu ambao si Waislamu ni Wakristo." Sheikh Ngao alikiri kwamba uvamizi huo ulielekezwa kwa kundi lisilohusika.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni