Ijumaa, 3 Agosti 2012

MFAHAMU MCH JOHN WA TAG UGALA TABORA AMBAYE YESU ALIMPONYA UKIMWI

mwezi ulipita nilikutana na kijana anayeitwa John yeye amezaliwa huko Ugala mkoa wa Tabora katika kijiji chao wanalima sana Tumbaku na ndiyo zao linalowaingizia fedha hata kuwa na maisha mazuri. kama tunavyojua ujana tena alikuwa ni kijana waliyependa anasa na mbabe alifanya kila alichoweza alitembea na kila msichana aliyemtaka, na aliweza kufanya chochote alichotaka na alionekana ni kijana mtata sana na kila alipopita mahali watu walijua huko aendako lazima watasikia tu tukio lolote iwe ni ugomvi au jambo lolote tu. pamoja na kuwa alikuwa ni mkristo lakini alikuwa ni mbezaji sana wa walokole. alifanya hivyo hata vijiji vya jirani walimtambua kwa kufanya hivyo akajikuta akiangukia kwenye gonjwa la Ukimwi.
Mch John akiwa na mke wake kwenye harusi iliyofungwa Dar mwezi uliopita
safari yake ya kwenda kwenye uchungaji ni kama ndoto vile maana ana mdogo wake ambaye anaitwa Peter yeye ameokoka muda mrefu kidogo na kila akiongea na kaka yake kuhusu wokovu alionekana kama amechelewa. mdogo wake alikuwa na uchungu kuhusu watu wa kijiji kwao na akafanya kila aliwezalo kutafuta mhubiri ambaye angesafiri naye kwenda mpaka kijijini kwao angalau watu wasikie habari njema za Yesu kristo.
Mwinjilisti kazimoto mwanzilisi wa kazi ya Ussoke
Peter alifanikiwa kuonana na Mwinjilisti Kazimoto amabye aliongea naye kuhusu kwenda kufanya mkutano wa injili kijiji kwao naye akakubali na kupanga safari na wakasafiri mpaka Kijiji cha Usoke ambako huyo kaka yake ana nyumba na Mwinjilisti huyu anafikia nyumbani kwa John ambaye ni wembe na ni lazima alete wanawake katika hiyo nyumba yake, kwa sababu mke wake aliyekuwa akiishi nae alisha faliki kutokana na Ukimwi miaka kadha iliyopita.
                                                            Mch John hapa alikuwa Dar
alivyoona mtumishi huyo amefikia nyumbani kwake kido wiki hiyo hakuleta wanawake wake lakini alimuona mdogo wake na mtumishi wa Mungu ni kama wamechelewa sana na hawana kazi ya kufanya. Peter alikodi nyombo na kufanya mkutano kwa umaskini sana maana uwezo wa mkutano mkubwa hakuna kiu yake watu wa kijijini kwao wasikie tu kile yeye alicho nacho(Yesu) mkutano ulikuwa mdogo lakini wenye utukufu wa Mungu na waliokoka watu wachache sana katika mkutano huo alikuwepo mama mmoja ambaye na yeye alikuwa ameokoka lakini mazingira yalikuwa yakimzonga sasa anapata mwamuko na kutiwa nguvu ya kusonga mbele katika wokovu.
           Mch  Kanemba wa TAG Magomeni anaye hudumia makanisa kadhaa mkoani Tabora

kwa sababu hakuna mchungaji mama huyo kwa sababu angalau alikuwa najuajua wokovu anaachiwa waongofu wale wachanga awalee!!!!. kazi ya Mungu inasonga mbele huku roho mtakatifu akiendelea kusema na John. baadae kanisa la Magomeni TAG liliamua kupeleka Mchungaji kutoka Dar kwenda Ussoke na anapofika kule anaifanya kazi ya pale kupata nguvu mpya watu wengi waliendelea kuokoka akiwamo John naye anaamua kuokoka huku akopata tumaini jipya kuwa bado yapo maisha ndani ya Yesu. mdogo wake baada ya kusikia kuwa kaka yake ameokoka alifurahi sana na kumuagiza kuja Dar akutane na wachungaji ili kumjenga kiroho.
                      Mch Kabanda ambaye alipelekwa Ussoke kuimarisha kazi ya huko ni moto

 Mungu ni mkubwa katika hali yake ya kujijua kuwa yuko postive Yesu anamponya Ukimwi. kwake ulikuwa ni muujiza mkubwa ambao unamfanya abaki ya Yesu na kuanza kumhubiri bila haya na akabadilika na kuwa mtumishi mzuri wa kuwa leta watu kwa Yesu. kazi ya mungu ikazidi kusonga mbele na yeye pamoja na mch wake wanafanya kazi kwa pamoja kutafuka kondoo waliopotea. kazi inakuwa kubwa na vijiji vitatu sasa vinafikiwa na injili na ilimbidi Mchungaji ibada za katikati amwachie John ili kumsaidia.

                               Mch John akifanya huduma ya kuombea watu kijijini kwao Ugala

Mungu wetu ni wa huruma na upendo mwingi sana kwa John, John anafanyika msaada sana katika kazi ya mungu jamaa, marafiki na wote waliokuwa wana mjua wanahamaki kuona yule mbabe mbezaji wa walokole naye kaokoka! ilibidi wakubali baada ya kuona matendo ya John ni tofauti na awali. na kutokana hivyo aliomba kiwanja kijijini kwao ili wajenge kanisa. kweli kijiji kilitoa eka 2 na hata mimi nilifika na kuona kiwanja hicho kikubwa sana kwaajili ya kazi ya Mungu na kwa sababu ni pori ilibidi kuanza kufyeka na kuanza kufanya ibada chini ya mti mkubwa ulioko kwenye kiwanja hicho.

                                                     washirika wakiwa ibadani chini ya mti

Nifupishe tu kwa kusema Baada ya Mungu kuwa amemponya na yeye kuthitisha hivyo akaona si vyema aishi peke yake ili ampate msaidizi wake ndipo akamchumbia na kuoa na taratibu za TAG huwezi kufunga harusi bila kupima Ukimwi vipimo vilionyesha ni mzima na akafunga harusi hapahapa Dar. na sasa yuko huko Ugala mkoani Tabora akiendelea kumtumikia Mungu. Jamani Mungu anaponya ukimwi si hadithi wala ndoto ni halisi kabisa ukiamua kumpa yesu maisha yako atatakasa kabisa damu yako nayo itakuwa safi kabisa.
                                                   Mchungaji John na mama Mchungaji

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni