Jumanne, 7 Agosti 2012

MAJAMBAZI WAVAMIA OFISI ASKOFU MKUU WA KANISA LA TAG. WAHARIBU VITU NA KUIBA LAPTOP 3

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia ofisi za kanisa la TAG makao makuu na kuiba. taarifa zilizoifikia blog hii watu hao walivamia juzi usiku na kuwafunga kwa kamba walinzi waliokuwa zamu kwa kama na hatimae kuvunja milango mbali mbali za makao makuu ikiwemo ofisi ya askofu mkuu na kuharibu milango ya makabati na madroo.
Askofu Mkuu wa TAG

watu hao waliweza kufanikiwa kuiba laptop 3 katika ofisi hizo na hatimaye walivamia na ofisi za kanisa la TAG Ubungo nako walifanya uharibifu na kufanikiwa kuiba sefu la hela na kuondoka nalo. sefu hilo la hela inasadikika lilikuwa na hela za ujenzi za kanisa hilo la TAG Ubungo zinazokadiliwa kufika sh milioni 6 pamoja na hela za mafungu ya kumi na sadaka ambazo hazikujulikana mara moja ilikuwa ni kiasi gani.

habari zaidi zinasema baadae sefu hilo likutwa limetupwa maeneo ya Kigogo na huku likiwa limevunjwa na kuchukuliwa pesa zote zilizokuwemo kwenye sefu hilo. walinzi waliokuwepo usiku huo hawakupata majeraha yoyote.

pamoja na wizi huo lakini leo ndiyo baadhi ya wajumbe wanaendelea kwenda katika mkutano mkuu wa kanisa la TAG unaofanyika Dodoma ambako kufanyika uchaguzi katika nyadhifa mbalimbali.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni