Jumatano, 8 Agosti 2012

WATU WENGI WAJITOKEZA KUPIMA MACHO KWENYE LOVE TANZANIA FESTIVAL

watu wengi wamejitokeza kwenye huduma ya upimaji macho na ugawaji miwani unaofanywa na huduma ya ipende Tanzania, inayotolewa katika vituo mbalimbali vilivyopangwa. timu ya madaktali wa kitanzania na wale wa kutoka Marekani imebidi watoe no maalumu ili kuweza kuhudumia watu kwa kufuata utaratibu. habari zilizoifikia blog hii zinasema katika kituo cha Magomeni watu wanaohudumiwa kwa siku ni 500. leo asubuhi kufikia saa 12:15 alfajili teyari watu 300 walisha jiandikisha watu wanafika mapema ili kuwahi foleni ijapo huduma zenyewe zinaanza kutolewa saa 3 asubuhi, hii ni kutokana na watu wengi kuwa na matatizo ya macho na inaonekana huduma hizi zimekuwa ni za aghali na ndo maana watu wengi wamefaidika na huduma hii ya kupewa miwani bure.
Masanja mkandamizaji akiwa na Andrew Palau

 bei za miwani ziko juu kuanzia 60,000 na kuendelea sasa kwa mtu wa kipato cha chini inakuwa ngumu kumudu, watu wengi wa kila lika wamefurahishwa na mpango huu amabao mwisho itakuwa kesho kutwa Ijumaa ukitaka kujua kituo kilichokaribu na wewe fuata link hii hapa http://www.martmalecela.blogspot.com/2012/08/love-tanzania-festival-waendelea-na.html

ukiachilia mbali utoaji wa miwani huduma nyingine jana ziliendelea na maandalizi nayo yanaendelea kwaajili ya uhitimishaji wa sherehe hizi jumamosi na jumapili pale jangwani. angalia baadhi ya matukio katika picha.

Askofu Imalasusa akiongea na waandishi wa habariKAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni