Jumanne, 7 Agosti 2012

LOVE TANZANIA FESTIVAL WAENDELEA NA HUDUMA MBALIMBALI KATIKA JIJI LA DAR JE UNA TATIZO LA MACHO KAPIME NA UPEWE MIWANI BURE!!!!

Love Tanzania festival inayoongozwa na Andrew Palau  wanaeendelea na huduma mbalimbali katika jamii ya wakazi wa jiji la Dar. kuanzia jana kuna madaktari wa macho kutoka Marekani na wa hapa Tanzania ambao wako kwenye vituo mbalimbali kwa ajili ya kuwapima watu wenye matatizo ya macho na watakao hitaji miwani basi wana pewa miwani bure kabisa miwani inatarajiwa kugawiwa ni kama 10,000 hivi.
Huduma kwa wanafunzi


Kuanzia August 6-10 Love Tanzania Festival (Tamasha la Ipende Tanzania) inatatoa huduma 4 za bure za vipimo vya miwani za kusomea. Tafadhali tusaidie kufikisha taarifa kwa watu wanao toka jirani na maeneo yafuatayo. Huduma hizi zinatolewa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka kumi jioni kila siku. Waganga wataalamu wakujitolea watakuwa wakitoa huduma hizo. Ni wakati wa kuipenda Tanzania!
maeneo miwani inako gawiwa ni
 1. TAG Church Mbagala
2. Baptist Mission Church - Magomeni
3. Lutheran Church - Vinguguti
4. St. Nicholas Anglican Church - Ilala Amana


ukiachilia mbali huduma hiyo ya miwani kumekuwa na ushuhudiaji na ufundishaji wa vitu vingi amabavyo vinafanywa na watu wa huduma hiyo katika mashule na sehemu za wazi.
Watumishi wa Mungu wakihubiri hapa na Maeneo ya Magomeni


ratiba ya leo pamoja na kuendelea kugawa miwani Andrew Palau Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Confference) katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
                            Mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo

 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.

Tuendee kuombea na kushiriki katika huduma hii tutakuwa tukikuletea matukio mbali mbali yanayoendelea sehemu mbalimbali za jiji la Dar. lakini usisahau kikomo cha haya yote ni kwenye viwanja vya jangani jumamosi na jumapili usitamani kukosa unaweza kutembelea link hizi hapa chini.KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni