Jumanne, 28 Agosti 2012

WATANZANIA WAFULIKA KATIKA UKUMBI WA VIP-DIAMOND JUBILEE KWAAJILI YA KUONANA NA WAINJILISTI KUTOKA SCOAN LAGOS KWA NABII T.B. JOSHUA

 

Watanzania wametokea kufurahia sana ugeni uliofika nchini kwetu kutoka kwa Nabii TB Joshua asubuhi ya jana katika ukumbi wa VIP Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Zoezi zima lilikuwa la kujiandikisha majina kwa wale wagonjwa wanaotaka kwenda Nigeria kuombewa na Nabii TB Joshua. Zoezi lilianza asubuhi saa 1:00 na kuendelea.

Kuna vigezo ambavyo vinahitajika kwa wale wanaotaka kwenda kuponywa naYesu kwa kupitia Nabii TB Joshua. Vigezo hivyo ni:-

MOJA// Medica Report kutoka kwa daktari isiyozidi miezi sita tangia umepewa.
Kama huna hiyo ripoti au unayo lakini ni ya muda unaozidi miezi 6, unatakiwa kwenda kwa daktari ili upewe nyingine.

MBILI// Mume au Mke anayehitaji mtoto.
Ithibitishwe kuwa ni kweli humjawahi kupata mtoto tangia mumeoana.

TATU// Wale ambao wana matatizo ya kutokuwa na mbegu za kiume, wanahitajika kupiga Utra Sound au kuskaniwa katika hospitali za serikali na sio za watu binafsi, baada ya hapo upeleke hiyo ripoti.

NNE// Watu wenye HIV AIDS wanahitajika kuleta ripoti kutoka katika hospitali za serikali.

Leo  watakuwepo tena katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Salaam kuanzia asubuhi.

Watanzania wakiwa katika ukumbi wa VIP Diamond Jubilee.
Akina mama na wadada wakifuata mstariari kwenda kutoa ripoti zao kwa Wainjilisti
Huyo mzungu ni mmoja wa Wainjilisti kutoka SCOAN akihakikisha watu wanafuata foleni.

Watu wakisubiria huku wakiangalia Video mpya ya Wise Man Harry aliyeenda Marekani na kufanya mambo makubwa huko kwa utukufu wa MUngu
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni