Ijumaa, 10 Agosti 2012

AJALI YAUA WANAKWAYA 12 MTO WAMI WALIKUWA WANATOKA KENYA KUJA DAR

Ajali nyingine mbaya imetokea maeneo ya Wami mkoani Pwani na kuua raia 12  kutoka Nchini Kenya

Na tayari Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ameagiza Serikali ya nchi hiyo kuileta ndege nchini Tanzania kuchukua majeruhi.

Tanzania imekuwa ikishuhudia ajali nyingi mbaya na zakusikitisha ambazo zimekuwa zikipoteza nguvu kazi ya taifa.

Je ni kweli kwamba serikali imeshindwa kabisa kupata mwarobaini wa ajali hizi?
Lori lililogonga mabasi mawili mtot wamiMarafiki wa Tajua nini. mawazo yetu juu ya mwarobaini wa ajali hizi ambazo zimetupotezea ndugu zetu wengi na wengine kuwaacha wakiwa na vilema vya maisha. HABARI ZA UHAKIKA ZINASEMA-------Wakenya Waliokuwa Wanakuja Kwenye Mabasi Mawili Walikuwa Ni Wageni wa Kanisa la Presibiterian pale St. Columbus Palm Beach lililo chini ya Pastor Fredy Kyala HAWAKUWA wa Festival....Kwanini Watu Wanaunganisha na Festival???Pastor Freddie Japhet Kyara ni Kati ya Wadau Wakubwa Sana Sana Wa Festival ndiye amekuwa akizunguka na Palau katika Kutafsiri hata CCC alikuwa nae....Ndio maana Watu wanasema ni Wageni wa Festival kwa namna nyingine ilikuwa pia wawepo kwenye festival , Ndio Maana Taarifa zinasema walikuwa wanakuja kwenye KONGAMANO hilo la Pastor Kyala.....Mungu awe Mfariji wa Ndugu zetu wakenya.....Asante Harvest Mariki pamoja Prosper Alfred Mwakitalima kazi njema, tuendelee na kazi zingine za habari

Gazeti la habari leo limeandika hivi jinsi ajali ilivyotokea

WAKATI wanakwaya 12 wa dhehebu la kikristo walikufa papo hapo jana kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika Kijiji cha Makole jirani na Mto Wami na kuhusisha magari manne, Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ametuma ndege ya kuwabeba majeruhi wa ajali hiyo na kuwakimbiza Kenya kwa matibabu zaidi.
Katika tukio la ajali, wanakwaya hao 11 walikufa na wengine 25 walijeruhiwa vibaya baada ya magari manne yakiwemo mawili ya abiria yaliyowabeba wanakwaya hao kupinduka na lingine kugongwa na lori ambalo nalo liligonga lori lingine baada ya kusababisha ajali hiyo.
Akizungumzia chanzo cha ajali, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema ajali hiyo ilitokea saa 11 alfajiri jana ambapo lori la mizigo lililokuwa likitokea Tanga kuelekea Dar es Salaam liligonga basi dogo la abiria lililowabeba wanakwaya hao waliokuwa wakitokea Nairobi kwenda Dar es Salaam kwa shughuli za kidini.
Kamanda Mangu alisema lori hilo lililigonga basi hilo dogo baada ya basi hilo kusimama ili kutoa msaada kwa wanakwaya waliokuwa kwenye basi lingine lililokuwa mbele ambalo liliacha njia na kupinduka upande wa kulia wa barabara hiyo kwa chanzo ambacho bado kujulikana.
“Basi hilo lilisimama na abiria waliteremka ili kutoa msaada kwa wenzao ambao basi lao lilikuwa limepinduka upande wa kulia wa barabara ukitokea Tanga. Wakati wakiendelea kufanya uokozi ghafla likaja lori lililokuwa linatoka Tanga kwenda Dar es Salaam likaligonga basi lile dogo lililokuwa limesimama.
“Wakati dereva wa lori anajaribu kulimiliki lori hilo ili litulie barabarani, ghafla alijikuta akigongana uso kwa uso na lori lingine ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha.
Tukio hilo limesababisha wanakwaya 11 ambao ni raia wa Kenya kufa papo hapo na wengine 25, kujeruhiwa vibaya,” alisema Kamanda Mangu.
Kamanda huyo alisema kutokana na ajali hiyo, magari yaliyokuwa yakisafiri kati ya Dar es Salam na mikoa ya Kaskazini zikiwemo pia nchi jirani za Kenya na Uganda yalishindwa kupita katika eneo hilo kutokana na malori hayo kufunga njia na hadi jana mchana jitihada za kuyaondoa malori hayo zilikuwa zinafanywa.
“Tunaendelea kutafuta ufumbuzi ili kuyaondoa malori hayo na magari yaweze kupita, tuna uhakika wa kukamilisha kazi hiyo mchana huu,” alisema Kamanda Mangu.
Kuhusu marehemu waliokufa katika ajali hiyo, Kamanda Mangu alisema walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huku majeruhi wakikimbizwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha na wengine Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Taarifa tulizopata baadaye zilisema kwamba majeruhi waliofikishwa Kibaha nao walipelekwa Muhimbili baada ya kufanyiwa huduma za kwanza. Alisema dereva wa lori aliyeligonga basi hilo dogo la abiria anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Wakati huo huo, habari kutoka Kenya, zilizopatikana jana zilisema Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ameagiza ndege za nchi hiyo kuja Tanzania kuwabeba majeruhi na kuwakimbiza katika hopitali za Kenya kwa matibabu zaidi. Hata hivyo habari hizo hazikueleza ni lini ndege hizo zitawasili nchini ili kuwachukua majeruhi hao.
Wakati huo huo, John Nditi anaripoti kutoka Morogoro kwamba abiria 29 kati ya 51 wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kutokana na kupata majereha baada ya kutokea ajali ya mabasi matatu katika eneo la Makunganya , Wilayani Morogoro kwenye Barabara Kuu ya Morogoro- Dodoma.
Ajali hizo zilitokea jana kati ya saa 2: 50 asubuhi, ambapo ajali ya kwanza ilihusisha basi la Shabiby lenye namba za usajili T 425 BYS likitokea mkoani Dodoma kwenda jijini Dar es Salaam ambalo lilianguka na kuziba njia.
Wakati Basi hilo likiwa bado limeziba njia kwenye kona muda mfupi baadaye likatokea basi la Sumry lenye namba T 777 BWL aina ya Yutong kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza lilishindwa kusimama na kwenda kujikita korongoni.
Kama haitoshi, Basi jingine la kampuni ya Allys Sports Bus lenye namba za usajili T 692 BKV nalo likifuata nyuma ya Sumry naye alishindwa kusimama na kuangua kiubavu pia katika eneo hilo. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Leonard Gyindo na timu ya uokoaji walifika asubuhi hiyo eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hizo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa huo, kuwa ajali hizo zilitokana na uzembe wa madereva na mwendo kasi .
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya, alikiri kupokea majeruhi 51 kati ya hao 29 wamelazwa katika wodi mbili tofauti wakiendelea vizuri na matibabu.
“ Tumepokea majeruhi 51 kati ya hao 22 wametibiwa na kuruhusiwa na wengine 29 tumewalaza wakiwemo wanaume 7 na waliobakia ni wanawake na watoto wadogo, ambao hali zao zinaendelea vizuri , isipo watu wawili ndio wameonekana wameumia kwa kiwango kikubwa “ alisema Dk Lyamuya.
Naye mmoja wa mashuhuda wa ajali ya kwanza , Edward Chiutila, alisema huwenda ajali hiyo imechangiwa na utelezi kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha asubuhi hiyo kwa vile derava wake hakuwa katika mwendo kasi.
“ Nilikuwa mtu wa kwanza kwenda kuwasaidia kuwatoa majeruhi kwenye basi la Shabiby , lilikuwa ni eneo tambalale ...huenda utelezi umechangia kuanguka kwake” alisema Chitula aliyeshuhudia ajali hiyo.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni