Jumanne, 31 Julai 2012

WANAKWAYA WAPATA AJALI, 8 WAFA

WANAKWAYA wanane wa Maskati wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, 8 wamekufa na wengine 13 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa, Leonard Gindo amesema, ajali hiyo ilitokea Julai 28 saa 3:30 asubuhi katika Kijiji cha Magunge katika barabara ya Maskati Turiani wilayani Mvomero.
Gindo alilitaja gari lililohusika katika ajali hiyo kuwa ni lenye namba za usajili T575 AXY, aina ya Toyota Land Cruiser Pick Up, mali ya Kanisa Katoliki iliyokuwa ikiendeshwa na Padri Deogratias Mdewa ikitokea Maskati kuelekea Chogoali ilipofika eneo hilo iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo hivyo.

Amewataja waliokufa kuwa ni Teophila Jeremia (30), Godfrey Joseph (21), Leticia Claud (22), Cecilia Isaya (20), Elizabeth Wiliam (9), Elizabeth Jacob (21), Flugencius Lucas (23) na mtoto wa mwaka mmoja na nusu, Lilian Thomas.

Aidha, aliwataja majeruhi kuwa ni Stepines Isaya (22), Joseph Peter (32), Maria Isdory (15), Frank Pasian (19), Deus Gasper (18), Averine Karol (30), Hilda Hilary (28), Catherine Karol, Indence Jeremia, Mariam Jeremia, Hilda, Frolven pamoja na dereva wa gari hilo.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi pamoja na abiria kuzidi uwezo wa gari hilo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni