Ijumaa, 27 Julai 2012

WACHUNGAJI WOTE WA UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE MNAALIKWA KWENYE MKESHA WENU. UTAFANYIKA DPC KINONDONI

Mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya kipentekoste Mch Mwakibolwa leo wamewataka wachungaji wote amabao wako chini ya umoja huo kukumbuka ratiba ya mkesha waliojiweke ya kila mwezi. ameseka kila jnne ya mwisho wa mwezi huwa wanakuwa na mkesha. mkesha wa safari hii utafanyika katika kanisa la DPC Kinondoni (karibu na soko la TX)

amesema kuna mambo mengi kama wachungaji ya kuomba pamoja yanayohusu kanisa na Taifa kwa ujumla. jambo la 2 kutakuwa na wataalamu wa uchambuzi wa katiba na wataleta mapendekezo ya katiba itasomwa na wataruhusiwa kutoa maoni yao na kama kuna marekebisho basi watatoa hapo hapo.

kuhamasisha wachungaji ambao bado hawajapata barua za rais za sheria bila kushurutishwa inawezekana, basi wasikose watapewa hapo hapo mkesha unatarajiwa kufanyiaka kuanzia saa 3 za usiku na wachungaji pamoja na watu wote wafike kwa wingi na kwa kuwahi bila kukosa.

washirika mnaombwa kuwakumbusha wachungaji wenu ili wasikose.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni