Ijumaa, 27 Julai 2012

WANA WA INJILI KUTOKA TAG MAGOMENI WAFANYA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA MH SITA HUKO TABORA WATU 116 WAOKOKA MWANAMKE MMOJA ALIYEKUWA AMEOLEWA NA JINI AFUNGULIWA.

Timu ya uinjilisti ya watu 8 kutoka kanisa la TAG magomeni imerejea salama kutoka katika vijiji vya Urambo Tabora ambako walienda kwenye huduma. huduma hiyo ya mikutano ya injili ambayo ilianzishwa na chama cha vijana CA's mwaka 2005 na sasa inaendelezwa kufanya na kamati ya uinjilsti ya kanisa, kwa miaka yote hiyo imeweza  kufanya mikutano mbalimbali katika mikoa ya Dar, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma nk. walifikia kwenye kijiji cha Ussoke ambako kwa sasa kuna tawi la TAG Magomeni, na kilifanya mikutano katika vijiji vya Ushisha ambako kulifanyika mkutano kwa siku 2 na kijiji cha Ugala ambako nako kulikwa na mkutano wa siku 2.
wana wa Injili wakiwa wameshuka toka Dar
huu ndiyo usafiri wa kawaida kule Ussoke power Tiller

watu wakisikiliza mahubiri katika kijiji na Ushisha
katika kijiji cha ugala Mungu alitenda miujiza sana, mimi bloger nasimulia maana nilikuwa ni mojawapo ambaye nilikuwepo kwenye safari hiyo, kulikuwa na dada mmoja ambaye aliletwa na mume wake kufanyiwa maombi na alikuwa na mapepo, yeye alikuwa anajijua alisimulia kuwa hilo jini lilikuwa limemwoa na lilikuwa linamjia akiwa usingizini na kufanya nalo tendo la ndoa, hata wakati mwingi alikuwa akichelewa kurudi nyumbani lilikuwa likimpigia simu kwenye simu yake na kumwambia kwa ukali kuwa awahi nyumbani. ukiacha huyo watu wengi walifunguliwa na kuokoka. pamoja na kufanya mkutano lakini wana wa injili tulipata nafasi ya kutembelea eneo la eka 2 walizokuwa wamepewa kanisa ili waweze kuabudia na kwakweli walikuwa wanaabudia chini ya mti hivyo wana wa injili wajitolea sh 60,000 ili lijengwe bada la nyasi ili wasalie kwenye kimvuli.
           Mch John wa kanisa la TAG Ugala akifanya maombezi kwa watu waliofika kwenye mkutano.
Umati wa watu wakiwa kwenye mkutano

                   mwenye mapepo akiomewa na wahudumu kwenye mkutano kwenye kijiji cha ugala

                          Mwinjilisti Kazimoto ambaye alikuwa anahubiri kwenye mikutano hiyo

                                                kanisa la Ugala wanaosalia chini ya mti

                                       majivu ya nyasi za kanisa ambazo zilichomwa moto
                      

na wakati ujenzi wa banda hilo shetani kwa kutumia watu wake na kuleta fujo katika eneo la kanisa na kuchoma nyasi, lakini Mungu mkubwa mhusika alipatikana na aliamrishwa na kijiji ajenge sasa kwa ghalama zake. watu wa mahali hapa walikuwa na kiu sana ya injili. baada ya hapa tulifanya mkutano mwingine kwenye kijiji cha ussoke kwa siku 4 ambako nako mungu alionekana sana
                      watu wakikata shauri kwenye mkutano wa injili katika kijiji cha Ussoke

  Mwinjilisti Enocky Kipwate akichukua matukio ya mikutano hiyo
                            
katika mkutano huo pia kulikuwa na kwaya ya EAGT Urambo ambayo nayo ilifanyika baraka katika mikutano hiyo. ni ratiba ambayo ni endelevu ya kupeleka injili kama una mchango wowote wa mawazo au kifedha ili kupeleka injili ya Yesu mbele basi unaweza wasiliana na Mkurugenzi wa Kamati ya Uinjilsti ndugu Enecky Kipwate kwa no 0786406411 Mbarikiwe sana.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni