Ijumaa, 27 Julai 2012

PASTOR MYAMBA ASEMA YEYE SI FREEMASON, KAMA KANUMBA AFINGEKUFA NAYE ANGEIGIZA NDANI YA GOD KINGDOM, FILAMU ZAKE ZINAMAFUNDISHO YA KIMUNGU

Yule mwigizaji nguli wa filamu anayejulikana kwa jina la Pastor Muyamba amesema kuwa yeye si Freemasoni na hataki kuzungumzia swala hilo kwani freemasoni ni nani? mbona ni kitu kidogo sana kwake yeye amelibeba jina kuu la Yesu sema watu wamekuwa na hofu tu lakini hakuna chochote. hayo aliyasema katika kipindi cha inuka uangaze cha praise power radio.

 
Pastor Myamba hivi karibuni atatoa Filamu yake mpya ya {GOD"S KINGDOM} aliyo fanya na Kampuni yake ya {Bornagain Films Production}Ni Filamu inayo onyesha kazi ya kristo katika kuwaleta watu kwake, Ni Filamu iliyokuwa na Upako wa ajabu mana baadhi ya sehemu walizokuwa wakifanya shooting ilibidi kusimamisha ili Roho mtakatifu afanye kazi yake. akielezea filamu hiyo ambayo alisema kama The great Kanumba angekuwa hai basi naye angehusika kuigiza filamu hiyo kwani walishirikiana nae kuweka sawa baadhi sehemu.

katika kipindi hicho ambacho kilikuwa na mada inayosema NINI FAIDA YA FILAMU ZA KITANZANIA KWA MTU ALIYEOKOKA JE FILAMU HIZI ZINAWEZA KUMBADILISHA MTU ASIYEJUA WOKOVU?

akijibu alisema siyo filamu zote zinaweza kumbadilisha mtu. ila filamu anazotoa yeye zimaweza na ni maombi yake kuwa watu wabadilike na kumfuata Yesu kiu yake ni kuona Dunia inabadilika na kumwamini Mungu.

baadhi ya maswali yaliyoulizwa kwenye kipindi hicho kupitia facebook ni kama ifuatavyo


Johns Bobby Johns bobby wa temeke nilikuwa na muuliza mchungaji muyamba kuwa alishawai kufikiria kuimba nyimbo za kuabudu kama alivyo fanya masanja wa ze comedy.
 
JIBU akijibu alisema yeye hajawahi kuwaza kufanya kama Masanja kwani ana hisi sauti yake siyo nzuri ila kama siku sauti ikifunguka ataweza fanya hivyo


Noreen Aloyce mchungaji Mihyamba unategemea nini badaee katika uchungaji wako?

JIBU kama Bwana atasema na mimi ninaweza kuwa lakini kwa sasa niko kwenye kuigiza


Gudila Mtalo napenda sana kuangalia movie za pastor myamba, anaigiza vizuri sana ila nauliza kwanin iwadada wanaoigiza wanavaa nguo fupi sana hata mahali ambapo hatakiwi kuvaa hivo...

JIBU mimi katika filamu zangu huwezi kukuta vitu hivyo ukiona mtu kavaa nguo fupi ujue mahali hapo pamerazimu sana kufanya hivyo akizidi kujibu alisema kuwa hata katika chuo chake anawafundisha wanafunzi kuwa na maadili hasa katika mavazi.


Lusekelo George Wa mtoni kwa Aziz Ally. Kiukwel kuna baadhi ya muvi kama pastor miyamba, village pastor, devil kingdom zinaweza kumbadilisha mtu akaokoka. Ila muvi za aina hii ni chache nyingi zipo kidunia zaidi.
 
JIBU siwezi kuzizungumzia filamu nyingine na ndo maana yeye ameanzisha kampuni yake ili kuhakikisha anajitosheleza katika kutoa filamu zenye upako na alisema kuwa filamu zake asilimia 80 ni mafundisho ya kiroho na amekuwa akipata shuhuda ya watu kuponya na kuokoka baada ya kuangalia sinema zake kama Zanzibar na sehemu mbalimbali.
 
vile vile aliifafanua kuwa alianzisha chuo cha kupika mastar katika filamu na anashukuru kuwa wasanii wenzake wakubwa kama akina JB, Ray kwa sasa hawapokei mwigizaji mpya mpaka awe amepitia katika chuo chake ambacho kinatoa mafunzo kwa miezi 6 miezi 3 ya kwanza wanajifunza darasani lakini 3 minine unaenda katika uhalisia kuigiza na mastar katika filamu zao.
 
alifafanua kuwa watu wenye vipaji na wanaotaka kujiunga na chuo chake wana karibishwa sana ili kujiunga katika chuo chake cha TFTC kwa no 0712 723 600 au 0766 335 014 na watapata maelekezo namna ya kujiunga.
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni