Alhamisi, 19 Julai 2012

ORIJINO KOMEDI WATAOKOKA WOTE? MCH MWAKIBOLWA NI MFANO WA KUIGWA, WATU MAARUFU NA VIONGOZI NAO WANAMHITAJI YESU. KILICHOTOKEA MPAKA MASANJA KUAMUA KUOKOKA

watu wote walio okoka huwa tunapenda kuona watu maafuru au viongozi wenye nyazifa za juu waokoke! ni kweli jamani. lakini huwa hatuchukui hatua kuwaendea watu hao. leo ukiwauliza walokole kuwa mnataka Rais Kikwete aokoke? wote watajibu Ndiyoooooooooooooo kubwa. lakini Je ? ni nani atakaye thubutu kwenda kumshuhudia Rais Kikwete?. nimewaza tu mara nyingi huwa nasikia kuwa ana kutana na viongozi mbali mbali wa dini au anaalikwa kwenda kwenye uzinduzi wa makanisa kuwekwa wakfu maaskofu. katika risala zao sijawahi kusikia kuwa Raisi unatakiwa kuokoka maana mbele yako kuna Jehanamu ya moto! au sidhani kama imewahi tokea kuwa mtu akaomba apointment na Rais au waziri harafu akifika aanze kumshuhudia habari za Yesu na kumsisitiza kiongozi huyo aokoke. kama hatujawahi kufanya hivyo huu ni udhaifu na ninafikiri kuwa roho za vigogo hawa zitakuja daiwa mikononi mwetu.

ni muda sasa kuanzia nimesikia kuwa mchekeshaji maarufu Masanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi kama wanavyojiita wao, kuwa ameokoka na hivi karibuni ametoa albamu yake ya nyimbo za Injili. nahisi inaweza kuwa lango na wenzake kufuata nyayo zake nao kuokoka, nimefuatilia na kupata kujua aliokokaje na nikavutiwa ha habari hivyo nakuona inaweza kuwa changamoto kwetu namna ya kuweza kuwafikia watu maarufu ili nao waweze kuokoka pia .

Mch mtarajiwa Masanja akiwa na Mch Mwakibolwa wa mito ya Baraka

Kuokoka kwa masanya kulikuwa hivi. akieleza njinsi masanja alivyookoka Mch wa kanisa la mito ya Baraka Mwakibolwa alisema kuwa alijua kuwa Masanja ana kitu na Mungu anaweza kumtumia katika kuvuna roho za watu, hivyo alichofanya alianza kumkaribisha kwenye ibada za kanisani kwake kuanzia mwaka 2007, bila kuchoka wala kukata tama aliendelea mpaka ilipofika mwaka 2010 ndipo Masanja yeye mwenyewe alipokata shauri na kuamua kuokoka na kukubali kubatizwa kwa maji mengi na kuanza kutangaza hadharani kuwa ameokoka. ilichukua miaka 3, ya kufuatiliwa na kukaribishwa kanisani na Mchungaji mwakibolwa, Hapa kwa kibinadamu Mchungaji anastahili pongezi kwa kuona kwa jicho la tofauti kile kilichokuwa nadani ya masanja na matunda yake yanaonekana sasa, maana sasa hivi watu wengi wanamualika katika mikutano mikubwa ya ijili, kwenye makanisa yao na amekuwa akiwavuta wengi kwa Yesu.

Hapa akiwa Nzega kwenye mkutano mkubwa wa injili na Mtumishi wa Mungu Daniel Kulola

Kanisa lenyewe la mito ya baraka lina ratiba ya kila jumamosi kuzunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Dar na kuhubiri habari za Yesu na hapo masanja hakosemani na amekuwa akikusanya watu wengi sana na wengi wanampokea Yesu. soma hapo chini

http://mkandamizaji.blogspot.com/2011/04/kila-jumamosi-kanisa-letu-la-mito-ya.html

Albamu aliyoitoa ambayo nimeshuhudia ikifanya vizuri sokoni inaweza kufungua milango na kwa watu wengine kuweza kumpokea Yesu. katika albamu hiyo kuna wimbo anaonekana yupo MC Reagan na wengine kama akina Joti Mpoki sura zao hazimo kabisa sasa nani atafuata? yeye japo ameokoka bado anaigiza na anasema hata hiyo nayo ni kazi ijapo shauku yake ni kuwa mchungaji hadi kujiita ni mchungaji mtarajiwa anasema ataacha kuigiza komedi pale tu Mungu atakapo mwambia aache kama asipomwambia ataendelea tu .ni changamoto katika kuipeleka injili kwa watu wote bila kujali dini, vyeo au mazingira wanayoishi na tukifanya hivyo ninaamini tutakuwa na viongozi wengi wenye kuokoka na wenye hofu ya Mungu na kazi ni ni yetu sote. Ubarikiwe kama utaanza kufanya hivyo
Hapa akihudumu Madhabahuni kwenye mkutano

Hapa akihubiri kwenye mkutano Nzega
Hapa akiwa na Mtume Ndegi wa living water na Mchungaji wa kwenye maigizo Muyamba


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni