Jumatano, 18 Julai 2012

BILL CLINTON AMTEMBELEA MANDELA KIJIJINI KWAKE NI KATIKA KUSHEHEREKEA MIAKA 94 YA KUZALIWA KWA MANDELA: SIKU YAKE YA KUZALIWA YAWA NI SIKUKUU YA KIMATAIFA


Leo ni siku ya kuzaliwa ya rais wa kwanza mweusi kwa Afrika Kusini ndugu Nelsoni mandela. shamla shamla za kusheherekea siku hii zimeanza siku nyingi ambapo tar 29 Juni watu wengi walikusanyika katika viwanja vya ili kurekodi wimbo wa Birthday ya Mandela. leo saa 8:00 vituo vya redio watu walioko mitaani na mahotelini waliimba wimbo wa happy Birthday mandela. watoto wa shule wapatao milioni 12 wameimba wimbo wa birthday.


Rais wa wa zamani wa Marekani Bill Clinton ni kati ya watu maarufu waliofika kijijini Qunu, Eastern Cape kwa Mandela kusheherekea nae siku yake ya kuzaliwa. Clinton amesema anajisikia heshima sana kwani wakati yeye alipokuwa rais ya Marekani na Mandela ndiye alikuwa rais wa South afrika. Bill alikuwa na mwanae wa kike  Chelsea na walikaa saa moja na nusu huko kijijini alikozaliwa Mandela.

Mandela akiwa na familia yake

<><> KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Bill Clinton Rais wa zamani wa Marekani alipomtembela Mzee Mandela kijijini kwake hapo jana.

umoja wa mataifa umeitangaza siku ya kuzaliwa Mandela 18 July kuwa ni siku ya kutumikia jamii kwa kuwaonyesha wema watu wanaokuzunguka kwa dakika 67 kukumbuka utumishi wa madela kwa jamii wa miaka 67 zaidi kwa wanainchi wa South Afrika. mara ya mwisho Mandela kuonekana hadhalani ilikuwa ni kwenye ufunguzi wa kombe la Dunia lililofanyika South Afrika. familia yake wamekusanyika nyumbani kusheherekea na kuwatoa wasiwasi watu huwa afya yake iko imara kabisa.

Chapisha Maoni