Alhamisi, 26 Julai 2012

MTU ALIYEKUWA ANATUMIA MAJINI KUUWA WANYAMA WAKATI WA KUWINDA AOKOKA SASA HIVI AKIENDA KUWINDA WANYAMA WANA MKIMBIA

Nilipokuwa huko Tabora kwenye kijiji cha Ussoke nilikutana na ushuhuda wa ndugu Martin nami nimeona ni vyema nikushirikishe, yeye kwa sasa ameokoka na ni mshirika wa TAG Ussoke kanisa tulilofikia tulipokwenda kufanya mikutano ya Injili. nilipata muda wa kuongea naye na kumfanyia maombi baada ya kushuhudia. yeye kazi yake ni uwindaji na alikuwa anatumia mizimu aliyokuwa ameachiwa na wakienda kuwinda wakisha ona wanyama kuna maneno anatamuka na wanyama wanpigwa na butwa na wala hawaendi popote hivyo anaanza kuwapiga tu na wala hawakimbii mpaka akishaona idadi imetosha basi anatamka na wanyama wanaendelea na safari yao basi anawaambia wale alioenda nae wanaokota wale wanyama wote wanapakia kwenye gari wanaondoka.

na aliniambia alikuwa anafanya hivyo kwa aina zote za wanyama hata Tembo na hata kama wakienda na gari kubwa lazima lijae wanyama na haikuwahi kutokea kutokupata wanyama na kwake kulenga alikuwa fundi kwa wanyama hawa wadogo risasi moja ilikuwa inapiga hata wanyama 3, kila risasi na nyama wake kukosa kupiga mnyama anapofyatua risasi ilikuwa ni ndoto.

Ndugu Martin
 lakini Yesu ni wa upendo ameokoka na alisalimisha vitu vyote vya mizimu na kuchomwa moto na Mtumishi wa Mungu Kabanda Wa Ussoke TAG. na baada ya kuchoma wakati akilala usiku alikuwa akisikia harufu ya wanyama na wakati mwingine anasikia sauti za mizimu aliyokuwa ameizoea, na haikuishia hapo tu bali wale wenzake aliokuwa nao waliona watapata hasara kwa kumwacha aokoke hivyo kuna siku walikuja kufanya ibada ya matambiko nyumbani kwake kwa sababu aliwakatalia kuingia ndani basi walifanyia nje na ilimshumbua mwili ulikuwa una msisimka.

                                                         Mch Kabanda wa TAG Ussoke
siku iliyofuata walikuja tena na alienda kumwita mchungaji wakati wao wanaimba nyimbo zao nje ya nyumba yeye pamoja na Mch walianza kufanya maombi ndani ilichukua dakika 5 tano tu watu wote wa nje walitimuka wao wenyewe na haifahamiki ni nini kilichowafukuza hakijulikani. wakati nikiongea nae aliniambia tangu aokoke alisha enda mara 3 kuwinda na mara zote ametoka kapa hawajarudi na hata digidigi. anasema kwa sasa wanyama wakimuona wana mkimbia na mara ya mwisho alipowaona wanyama aliwaambia wenzake wamsubiri wakati amewakaribia wanyama na anataka aanze kufyatua risasi ataona wenzake wanakuja na wanyama wakatimuka alipowauliza kulikoni walimwambia kuwa tumesikia unatuita ndo maana tukaja.

pamoja na ushuhuda mrefu tulifanya nae maombi na anaendelea na Yesu wapendwa tuombe huko vijiji watu wana kiu sana na injili wewe hapa mjini kuna miundo mbinu inayokuwezesha hata kusikia neno la Mungu kuna sehemu nyingine wanatamani tuombe kazi ya Mungu isonge mbele. Amina
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni