Alhamisi, 26 Julai 2012

AISHI NA MWANAMKE AMBAYE NI JINI KWA MIAKA 3 AZAA NAE MTOTO! SIRI ILIFICHUKA SIKU YA HARUSI. MCHUNGAJI AFANYA MAOMBI YA SIKU 2 KIVUNJA NDOA HIYO

Kijana moja mkoani Iringa Ibrahimu Ng'onda anayesoma kidato cha nne katika secondary ya Efatha, alijikuta akiangukia katika mahuano na jini bila yeye kujua. akieleza kisa hicho baada ya kufanyiwa maombi ya nguvu yaliyomzindua kutoka katika hali ya kuzimia kwa siku mbili mfurulizo.

kisa chenyewe alieleza hivi alikutana na dada ambaye hatukupata jina lake mpaka tunaenda mitamboni ambaye alijitambulisha kuwa anasoma katika Chuo kikuu cha Tumaini Mjini Iringa, na walianza mahusiano ya kimapenzi, alitizimiwa kiasi chochote pesa alichokuwa anakihitaji na kutembea na huyo dada kwa kutumia gari yake na dada huyo alimwambia kuwa yeye mtoto wa tajiri asiwe na wasiwasi kwa habari ya pesa na mara zote alipokuwa anamwomba pesa alimwambia achukukue kwenye dro ya gari ambayo ilikuwa na pesa nyingi.

na ilifika kipidi huyo dada alipata mtoto na kujifungua mtoto wa kiume, ambaye kwa sasa alikuwa ametimiza miaka 3 mwaka huu wakati kijana akijianda na mitihani kwaajiri ya kupita ili afanye mitihani ya kidato cha nne yule mke wake alimuletea mihani yote na kumtaka aisome ili asifeli. lakini Ibrahimu alikataa na kumwambia kua anataka ajipime akili yake bila kutumia msaada wowote, baada ya kukataa huo msaada yule mwanamke akamwambia basi ujue utafeli na kweli kijana baada ya kuanza mitihani alikuwa haelewi kitu kabisa na kujikuta kufeli sana. na alipokutana na huyo mdada akamwambia habari za mtihani yule mdada akamwambia mi si nilikwambia kuwa utafeli umeona sasa. yule kijana akahamaki kupata jibu hilo na kumuuliza we jini nini?!! yule mdada akamjibu hata kama ukijua kuwa mimi ni jini utafanyaje to late.

kijana hakuwa na ujana wa kujinasua na akapewa sharti kuwa afuge kucha yake mmoja na asiikate mpaka atakapo mwambia, na kijana akafanya hivyo. ilipopita muda kama wiki tatu zilizopita akaambiwa aikate hiyo kucha na baada ya kuikata tu alizimia. (kilichomtokea yeye baada ya kuzimia nitakujuza baadae) baada ya siku 2 ndugu zake waliamua kumpeleka hospital alihudumiwa bila mafanikio, ndipo walipo kumbuka kuwa kuna walokole huwa wanaombea watu ndipo wakaenda kwa mtumishi wa Mungu Mch K. Emanuel wa kanisa la International Petecoste liloko Kihesa Lugalo Iringa mjini. baada ya kufika wakamwelezea basi wakaondoka nae mpaka hospital kwenye wodi aliyokuwa amelazwa.

baada ya kuanza kumfanyia maombi yule kijana akazinduka na akawa anawauliza likuwapi gari langu jipya la kifahali nililozawadiwa zikowapi hela zangu millioni 200 nilizopewa, ndugu zake wakabaki wana shangaa basi wagonjwa wengine walipoona yule mtu kazinduka wakaanza kumwita Mtumishi wa Mungu Ema ili awafanyie na wao maombi wakati anawafanyia maombi watu wengine Ibrahimu akazimia tena! ndipo Mch akawaambia wale ndugu zake kuwa wambebe na wampeleke kanisani kwa maaombi zaidi. sasa kwasababu walikuwa na shida ilibidi waingie kanisani ijapo wao ni waislamu, yakaanza maombi ya nguvu kwa muda wa siku 2 mfululizo.

 baadae mapepo yakaanza kuzungumza na kusema hayatoki maana kuna sherehe kubwa imeandaliwa kwaajili yake hawawezi kumwacha, lakini baada ya kukemea kwa muda mrefu yasema yanatoka, hatimaye kijana akazinduka na kuelezea kisa hiki na kusema wakati amezimia alikuwa nyumbani kwa jini na kulikuwa na sherehe kubwa ya harusi kati yake na huyo jini na alikuwa ameshapewa hela nyingi na gari la kifahari, na ndiyo maana alipozinduka kwa mara ya kwanza hospitalini aliviulizia! ndugu zake kusikia hayo walibaki midomo wazi na familia yote ya watu 10 wakaamua kuokoka japo ni waislamu tena swala 5 na wanaendelea na mafundisho,

 walimwita ndugu yao ambaye ni imamu huko ZNZ ijapo alikuwa anapinga ndugu zake wasiwe wakristo lakini nae amewaambia hao ndugu zake waendele maana Mungu ni mmoja na mambo hayo kwao yangekuwa magumu. pamoja na hayo yote lile jini lilikuwa bado linamtokea Ibrahimu huku likiwa na yule mtoto wao wa kiume na huku likiwa na majeraha sana, na kumwambia kuwa halikuwa na nia mbaya na yeye lilikuwa na nia ya kumlinda tu. huo ndiyo ushuhuda wa matendo makubwa ya jina la Yesu ambao umetendeka huko Iringa umaweza kuwasiliana na Mch Emanuel kwa  Namba yake ya simu ni  0713 053222. Ukiwasiliana nae utapata taarifa nzuri na sahihi zaidi, maana kuna mengine mengi sikuweza kuyaeleza. Mungu akubariki. na hata kama unahitaji maombi auushauri wa kiroho.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni