Alhamisi, 26 Julai 2012

BAADA YA KUPATA AJALI KIONGOZI WA THE VOICE. WADAU MNAOMBWA KUCHANGIA MATIBABU

kama una taarifa au kama hauna ndo ninakujuza kuwa kiongozi wa kundi la The Voice Obedi John Mark alipata ajali maeneo ya Sinza Kamanyola, akiwa na usafiri wa bajaji akiwa anaelekea Magomeni...Kwa sasa hali yake si nzuri yuko chini ya uangalizi wa Daktari Mvungi ndani ya Hopitali ya Kinondoni na ameumia sehemu za Kichwa. anaendelea na matibabu hadi jana zilikuwa zimesha tumika kama 400,000.
Obedi aliyepata ajali

watangazaji wa PPR Uncle Jimmy na Elic katika kipindi chao cha asubuhi Rise and Shine wamewaomba waimbaji wa muziki wa injili pamoja na wadau wote wa injili kujitoa katika kuchangia matibabu ya mwimbaji huyo. wametoa no ambazo watu wanaweza kuchangia kiasi chochote kuanzia sh 1000 na kuendelea nazo ni Mpesa 0764 993 982, tigo pesa 0568 334 797 na Airtel Money ni0784334797.

aitha wamewaomba waimbaji wote wa nyimbo za injili na wadau wenye nafasi wakutane pale PPR saa 5 ili waende kumuona mwimbaji huyo hospital. msafara huo utaongozwa na rais wa muziki wa injili ndugu Addo November


ni maombi yangu Mungu aendelee kuponya ili asikose kwenye lilee tamasha kubwa litakalofanyika mapema mwezi ujao
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni