Jumatatu, 11 Juni 2012

HALI NITETE NIGERIA MAKANISA MAWILI YALIPULIWA NA MABOMU JANA

Nigeria ni nchi ambayo kwa sasa imefikia pabaya kwani karibu kila wiki wakristo wamekuwa wakiuliwa. wiki mbili zilizopita kuna makanisa yalilipuliwa na watu waliokuwa na mabomu.  kabla hilo halijaisha zikatokea ajali mbili za ndege ikiwapo ndege ya abiria ambayo ilikuwa na abiria zaidi ya 150 na hakuna aliyesarimika kwenye ndege hivyo siku ya jumapili iliyopita.
Watu wakiangalia mabaki ya gari lililokuwa limebeba bomu
jana tena kuna makanisa mawili yameshambuliwa na mabomu na kuua watu kadhaa. habiri kutoka Nigeria zinasema makanisa yaliyolipuliwa yanatoka katika sehemu za Jos na Borno. habari zaidi zinasema mtu mmoja alijilipua na bomu katika lango kuu la kuingilia kanisa la  Christ Chosen Church of God lililoko Rukuba Road mlipuko huo pia uliathili kanisa la jirani la Evangelical Church of West Africa mtu huyo aliyekuja na gari aina ya Volkswagen alifika wakati 11:00 ambao huwa kuna  mkusanyiko wa watu wengine wanaokuwa wanatoka ibada ya kwanza na wengine wanaingia ibada ya pili. gari hiyo ambayo ilikuwa inaelekea kanisa la St. Peter’s Catholic Church lakini kulikuwa na vizuizi vilivyowekwa na vijana kwaajili ya ukaguzi ndipo akaamua kwenda kwenye hilo kanisa la Christ Chosen Church na kabla hajaingia ndani ya jengo bomu hilo lililipuka na  na kumuua mama mnoja hapo hapo lakini baadae ilipotiwa kwa watu zaidi ya 20 walikufa na watu kama 41 kujeruhiwa na kulazwa kwaajili ya matibu na sehemu ya jengo hilo lilibomoka. na kufanya vijana wa kanisa hilo kuweka ulinzi mkali.

Kanisa la Jos lililolipuliwa
Na huko Borno yameripotiwa matukio mawili la Biu na Borno State watu watano wenye siraha walikuwa nje ya  kanisa moja ambako walisubiri watu wanaanza kutoka ibadani wakaanza kuwamiminia risasi na kuingia hadi ndani ya kanisa na kuua baadhi ya washirika na kujeruhi watu wengi.

wakati huohuo kikundi cha kiislamu cha Maiduguri (AFP) – Islamist group Boko Haram kimekiri kuhusika na ulipuaji wa makanisa unaoendelea msemaji wa kikundi hicho aliwaambia waandishi wa habari kupitia simu, amesema wanafanya hivyo ili kuihakikishia serikali kuwa hakuwa ulinzi wowote wanao weza kuweka kuwazuia wao.

Askari wa kikundi cha kiislamu wakiwa na siraha nzito
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: