Ijumaa, 18 Mei 2012

UNAMKUMBUKA HAPPY KAMILI. YUKO STUDIO KUANDAA ALBAMU NYINGINE

Mwimbaji wa nyimbo za injili Happy Kamili kutoka Mbeya
Jina la Happy Kamili si geni katika tasmia ya muziki wa injili ijapo kwa mrefu sasa alikuwa kimya baada ya kutoa ile albamu yake ya kwanza, na wimbo uliomtambulisha ni ule wa Mpango wa Mungu ni lazima utimie, enzi hizo wimbo huo ulipigwa sana karibu katika kila kituo cha redio. sasa ameanza maandalizi ya kutoa albamu yake nyingine. Blog hii ilipata nafasi ya kufanya mazungumzo nae jana ili kujua kinachojili katika huduma yake ya uimbaji.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Happy Kamili kutoka Mbeya

Mwimbaji wa nyimbo za injili Happy Kamili kutoka Mbeya

kama nilivyokueleza hapo juu kuwa nilifanya nae hajiano. Mahojiano na blog hii yalikuwa kama ifuatavyo:-
Happy Kamili: habari za asubuhi
Martin Malecela: Nzuri mpendwa Bwana asifiwe
Happy Kamili: Amina
Martin Malecela: habari za siku
Happy Kamili: nzuri kaka unaendeleaje?
Martin Malecela: Mungu ni mwema huduma inasemaje? tunasubiri albamu yako nyingine au umestaafu kuimba?
Happy Kamili: Aah haiwezekani kuacha kuimba mpaka Yesu akija atanikuta naimba. lakini niko kwenye maandalizi niommbee
Martin Malecela: hamna shida maombi yangu utapata sana tu. unatarajia kuingia studio mwezi gani na unafikiria kurekodia wapi.
Happy Kamili: niko studio tayari nina nyimbo tano nimesharekodi, studio nimechanganya dar na mbeya
Martin Malecela: ok ubarikiwe sana tuliimiss sana sauti yako kumbe basi haitachukua muda mrefu kutoka?
Happy Kamili: hapana mwezi wa nane hivi itakuwa tayari
Martin Malecela: ok vip kuna waimbaji wengine ulioshirikiana nao ambao ni maarufu kama ulivyofanya kwenye albam yako ya kwanza kumshirikisa John Shabani
Happy Kamili: Hapana, nilie imbanae sasa hivi ni mdogo wangu
Martin Malecela: sijui kama umeipa jina
Happy Kamili: bado nafikiria.
Martin Malecela: ok ubarikiwe sana kwa taarifa nakuombea na ninakutakia maanadalizi mema ya hiyo albamu yako mpya
Happy Kamili: Asante
Martin Malecela: ok asante

wimbo uliosifika katika albamu yake ya kwanza ni Mpango wa Mungu ni lazima utimie huu hapa chini unaweza kupata radha yake halisi. na tunasubiri hiyo albamu yake inayokuja tuisikie na itujenge kiroho kwa utukufu wa Mungu.Pata na wimbo mwingine hapo chini unaoitwa siachi kamwe.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni