Jumatano, 2 Mei 2012

MCHUNGAJI YOUSEF NADARKHANI ANASUBIRIWA KUNYOGWA NCHINI IRAN NI MAOMBI YA WAPENDWA TU YANAHITAJIKA ZAIDI.

Wanasheria wa mchungaji Yousef Nadarkhani wa Iran wanasubiri uamuzi wa mwisho juu ya hukumu ya kunyongwa mpaka kufa, inayomkabiri mchungaji huyo.mwanasheria amesema hawajapata mawasiliano kutoka serikalini inayoonyesha  mteja wao atahumiwa lini, licha ya taarifa zinazovuma kuwa yuko karibu kunyongwa.
Uvumi wa utekelezaji wa kesi ya  Yousef Nadarkhani ulivuja wiki iliyopita baada ya chanzo cha karibu na mmoja wa wanasheria wanaoshugulikia kesi hiyo, kuwasiliana na vyombo vya habari vya kimataifa, na kuwaeleza kwamba mahakama ya Iran imeshatia saini kwenye karatasi ya Nadarkhani kwa utekelezaji wa adhabu yake ya kifo itafanyika hivi karibuni .

 MchYousef Nadarkhani na familia yake
Mwanasheria anasubiri uthibitisho tu, lakini anafahamu kuwa hati ya utekelezaji ilishatolewa, alisema Firouz Khandjani, ambae ni mwanachama wa baraza la madhehebu ya Kanisa la Iran. "Sasa sisi ni kujaribu kuelewa hasa ni nini kinaendelea. Sababu habari iliyokuja kutoka kwa mtu wa karibu na wakili, inatakiwa kuchukuliwa kwa umakini na kuifuatilia. Kesi Nadarkhani ilipelekwa kwa Kiongozi Mkuu Ayatollah Khamenei kwa ajili ya uamuzi juu hukumu ya kunyongwa, lakini kisheria mahakamani bado ina mamlaka ya kutoa amri ya utekelezaji, Khandjani alisema. Khamenei anaweza kufanya uamuzi wa kumnyonga , Ingawa wanasheria wa Nadarkhani hawajapata uthibitisho wa maandishi ya utekelezaji, Khandjani alisema kuwa wana wasiwasi  kwamba serikali haizitii Sheria zake yenyewe za kisheria katika kuwalinda wakristo.

Serikali ya Iran ina tabia ya kunyonga wafungwa bila taarifa, ingawa si ya kawaida.
"Tuna wasiwasi kwa usalama wa Wakristo Iran, kwa sababu serikali haiheshimu sheria au taratibu za kisheria," Khandjani alisema. "Tunasubiri uthibitisho, lakini tunapaswa kuchukua hatua, kwa sababu tunajua watu ambao wameuliwa bila taarifa.
Baadhi ya vyanzo vinasema vina  wasiwasi juu ya uhakika wa habari kwamba Nadarkhani yuko hai au la.
Mch Yousef Nadarkhani akiwa gerezani
Wakristo nchini Iran mara kwa mara hu kamatwa na kuhojiwa. Wengi wao ni watu wa mitandao ya makanisa ya nyumba kwa nyumba na makundi madogo madogo yanayokutana kwa siri
Mnamo Septemba 2010 Nadarkhani alihukumiwa kifo baada ya mahakama ya rufaa ya Rasht, 243 kilomita (maili 151) kaskazini magharibi mwa Tehran, kumkuta na hatia ya kuacha Uislamu na kubadili dini na kuwa mkristo. Amekuwa gerezani tangu Oktoba 2009. Ijapo taarifa za uhakika ambazo pastor huyo aliwahi kusema kuwa yeye hajawahi kuwa muuislam, wakristo ambao wako katika nchi za kiislamu wamekuwa wakinyanyaswa kwa kuwa ni wakristo, na jumuiya za kimataifa za haki za binadamu zimekuwa zikilaumu vitendo hivyo vya unyanyasaji wa wakristo. Wapendwa tumuombee huyu mchungaji mapenzi ya Mungu ya timie pamoja na wakristo walio kwenye nchi za kiislam.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Martha,
wewe unauhakika wa kile unachokieleza kuhusu kunyongwa kwa mchungaji huyo?