Jumatatu, 30 Aprili 2012

KITI NO 666 CHALETA UTATA NDANI YA BUNGE LA UMOJA WA ULAYA

Jengo kubwa la bunge la ulaya lenye mnara wa ajabu Duniani, lililotajwa kuwa ni mnara mwingine badala ule wa Babel, linalotumiwa na bunge la 5 la umoja wa ulaya lina kiti chenye no 666 ambacho kimebaki wazi bila kukaliwa na mtu kikisubiri mtu wa kukalia! Jengo hilo la peke lililopanda juu angani na kupata sifa , lililopo Brussels Ubeligiji  kwenye mlango mkubwa kuna bustani yenye sanamu ya mwanamke aliyepanda farasi, akiwa nusu uchi inayoelezwa kuwa ni ukamilifu wa unabii wa Biblia.
Jengo la bunge la Eu kwa njee
Katika jengo hilo la pekee kuna viti vizuri mfano wa viti vya kwenye ndege kubwa zinazopita anga la juu  na katika ukumbi huo kuna viti 785 ambavyo vimepangwa  nusu mduara na kila kiti kimeandikishwa jina la mbunge wa kukikalia, isipokuwa kiti no 666 ambacho kimebaki wazi. Uwazi wa kiti hicho umezua utata na maswali mengi  hasa kutokana na maelezo ya Biblia kuhusu no 666 Ufunuo 13, iliyotaja wazi kuwa itakuwa ni no ya kibinadamu. Katika hali ya kawaida kiti hicho kinachosadikiwa kuwa ni cha mpinga kristo kimekuwa wazi kwa muda sasa bila maelezo ya kina kwanini hakitumiki. Mpango wa viti hivyo vinavyozunguka kiti chenye no hiyo vimepewa majina kama ifuatavyo.
655 Couteaux
656 Fitzsimons
657 Hyland
658 Kuntz
659 De La Perriere
660 Marchiani
661 Montfort
662 Quiero
663 Souchet
664 Thomas-Mauro
665 Zissener
666 ----------------
667 Cappato
668 Turco
669 Bonino
670 Pannella
671 Dupuis
672Della Vedova
673 Dell'Alba
674Gorostiaga Atxalandabaso
675 Gobbo
676 Speroni
677 Bossi
678 Formentini
679 Crowley
Katika Biblia kitabu cha ufunuo 13:18 kinaeleza Neno la Mungu linasema hapo ndipo penye hekima, yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu na hesabu yake ni 666. Mchambuzi mmoja wa mambo ya kinabii amenukuliwa akisema leo hii maandiko hayo, yanatimizwa mbele za macho yetu. Kiti cha mpinga kristo kitakaliwa. Dunia inasubiri utimizo wa maendeleo ya mwisho, bwana atamuondosha kwa moto utakaotoka katika kinywa chake (neno la Mungu) na kwa nuru kuu ya kurudi kwake. Alisema kuwa jengo hilo kubwa la bunge la ulaya (the european union-EU parliament) linachukua wajumbe 785, liko brussels, ubelgiji. Ni zuri la ajabu ambalo halijawahi kutokea ndipo kuliko na kiti hicho kinachotarajiwa kuwa cha mpinga kristo. Umoja wa ulaya unatajwa kuwa eneo ambalo linaharakisha maandalizi ya kumpokea mpinga kristo. Anayetarajiwa kupitia utawala wa Rumi. Imetabiriwa kuwa ili uwe mwisho uwadie ni lazima ile rumi ya kale iliyoangushwa ifufuke upya. Ingawa umoja wa Ulaya in jumla ya wanachama 27 lakini wajumbe kamili ni 10 tu, na wengine hawana haki ya moja kwa moja. Kwa kadri ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, utimilizo wa yale yaliyotabiriwa unatimia kwa haraka sana huku baadhi ya mataifa yakianza kuingia katika hatua za mwisho za kutotumia fedha na badala yake watu wakipigwa chapa maalumu (micro-chip) hii ni kuelekea katiika jamii isiyotumia fedha(Cashless society)

http://www.jesus-is-savior.com/End%20of%20the%20World/seat_666.htm
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni