Alhamisi, 3 Mei 2012

KUKEFYAKEFYA (NAGGING) MITHARI 21:9

Kukefyakefya (nagging) ni nini?:
Ni kitendo cha kutafuta makosa na kuendelea kulaumu, kulalamika, kusumbua, kutesa, kuchokoza , kuudhi, kushutumu, kuleta mzozo ndani ya wanandoa.
Mara nyingi wanawake ndiyo wenye hii tabia ingawa imegundulika kwamba wapo wanaume wenye tabia hii pia  katika ndoa.


we ni wa kusemasema kila wakati duh
Pia kukefyakefya ni kitendo cha kumsumbua mwanaume kwa maswali, au kumtuma kitu au kumwambia afanye kitu kama vile ni bosi wa kihindi na mfanyakazi wake au mama na watoto wake wakati ni mke na mume ndani ya nyumba. Inawezekana mume wako anatabia ya kuacha bathroom kuwa chafu baada ya kutumia, akila anaacha meza na vyombo ovyo na vichafu, Inawezekana huwa anatupa nguo ovyo na kusambaa sakafuni utadhani chumba cha watoto wa shule, Inawezekana anakaa tu huku anazidi kunenepeana kama wachezaji wa sumo, au anaangalia TV kama vile ana mkataba na vituo vya TV na umekuwa unamwambia kubadilika lakini habadiliki na umeona dawa nikuendelea kumsema. Au umekuwa ni mwanamke mwenye maswali hata yasiyo na kichwa na miguu tangu asubuhi wewe ni kuuliza tu nakuendelea kuuliza.

"Unamuuliza, je Ulitoa zile takataka, ulilipa ile bill, umetengeneza lile dirisha, umemwambia fundi kuhusu tatizo la umeme hata hajajibu umeshampachika swali lingine"
Kawaida wanaume huwa hawapendi kuambiwa nini cha kufanya.

Kwa nini kukefyakefya si vizuri?
Kwa sababu husababisha mwanaume kukwazika, kwani hujiona yeye ni mtoto (child role) na mke ni mzazi au mama (parent role), Hakuna mwanaume anapenda mke wake kuwa kama mama yake mzazi. Mwanaume hujisikia haheshimiwi na mkewe (disrespectful)
Mwanaume hujisikia kushambuliwa na kudharauliwa nakujiona hafai (inadequate)

Kwa nini wanawawake hupenda tabia ya kukefyakefya?
Wanaume hawafanyi vile wanawake wanawaambia wafanye.
Pia wanawake hudhani kwa kurudia kukumbushia na kusutana basi mwanaume atafanya.
Wapo wanawake wamekulia mazingira ambayo mama zao walikuwa ni watu wa kukefyakefya kwa baba zao hivyo basi nao wanaamini hiyo ndiyo njia pekee ambayo wanaume wanaweza kufanya yale wanasema au wanataka wafanye.
Wengine ni asili yao kufanya hivyo.

Nini matokea ya tabia ya kukefyakefya?
Mwanaume huanza kumkwepa mke wake na kuchelewa kurudi nyumbani au kujibakia ofisini au kazini au kupitia sehemu hadi ahakikishe akirudi nyumbani mke amelala.
Mwanaume anaweza kuanza tabia mbaya za ulevi au kukosa uaminifu katika ndoa
Mwanaume huanza tabia ya kutosikiliza mke wake kwani anamchuja (filter) kwamba huyu ni tabia yake kukefyakefya so msumbufu.
Kuchokana katika ndoa maana hakuna ukaribu (intimacy) pamoja na mawasiliano kuwa ovyo maana mume sasa uwa si msikilizaji mzuri.
Mwanaume hukosa hamu na huyo mwanamke mwenye hii tabia.

Je, mwanamke afanyeje asiwe na tabia ya kukefyakefya?
Kwanza mwanamke lazima akubali kwamba yeye na mume wake wapo tofauti na azikubali tofauti, akubali upungufu uliopo na kuchukua maisha kama yalivyo.
Siku mwanaume akifanya vizuri ampe appreciation.
Lazima mwanamke awe positive kama mwanaume amefanya alichoambiwa afanye kwa maana kwamba usilaumu, shutumu, au kukasirika au kumfanya aonekane mpumbavu(stupid.)
Kawaida Hakuna kitu kibaya duniani kinachofanya tuone kitu ni kibaya bali ni jinsi tunavyofikiri (thinking)Shirikisha hisia zako kwake kama ungekuwa wewe kila siku unaambiwa kama mtoto mdogo ungejisikiaje.

Inawezekana mumeo huchelewa kurudi nyumbani au kukupa sababu eti anapitia sehemu kumbe anakwepa tabia yako ya kukefyakefya.
Ni afadhari kukaa kwenye jangwa kuliko mwanamke mgomvi na mchokozi(Mithali 21:19)
Ni afadhari kuishi pembe ya darini kuliko kukaa katika nyumba pana pamoja na mwanamke anayekefyakefya(Mithali 19:9)

Wanaume hawapendi Mwanamke Kulalamika (Mithari 21:19)

Ile unarudi tu home kutoka kazini kila siku jioni kiumbe huyu ndo anakutazama hivi?

Nahisi baada ya siku kadhaa utatamani urudi yeye tayari kalala!
Binadamu ni kiumbe anayependa sana kulalamika iwe ofisini, kanisani, hotelini, kazini, sokoni, darasani, mikutanoni, msibani, harusini nk watu ni kulalamika tu.

Na kwa upande wa wanandoa mwanamke ndiye anajulikana sana kwa kuwa mtu wa kulalamika kiasi kwamba wanaume wengi huwa wanachoka na kuanza kujiuliza hivi mwanamke anahitaji kitu gani maana kila unachompa bado hakiwezi kumfanya asilalamike zaidi au tena.


 Je, ni tabia ipi huchukiza wanaume?
Ukiwauliza wanaume wengi kwenye ndoa asilimia kubwa watasema hawapendi kabisa tabia ya mwanamke kulalamika kwa kila kitu na kwa wakati wote.

Kwa nini wanaume hawapendi mwanamke mlalamishi/mnung’unikaji?
Wanaume tangu watoto wao wamefundishwa kuwa tough, kuwa wavumilivu, kuwa unemotional, kuwa wanaume na zaidi kwamba tabia ya kulalamika si ya wanaume.
Matokeo yake wamekuwa watu dhaifu sana linapokuja suala la mtu mlalamikaji na hushindwa kuvumilia kuona mtu analalamika mnuda wote.
Wanaume pia ni watu wa ku-fix matatizo au kutoa solution na si kutafuta solution.

Mwanamke anapolalamika kwa mara ya kwanza humvuta mwanaume kuja kutatua tatizo na akiendelea kulalamika mwanaume hujisikia ameshindwa ku-fix hilo tatizo na hujiona failure mkubwa. Kulalamika si njia njema ya kuuliza au kupata kitu kwa mwanaume bali ni njia bora ya kumfanya ajisikie vibaya.

Mwanamke mlalamishi ndani ya nyuma kwa mumewe muda wote hufanya mwanaume amuone ni takataka zaidi na kwamba hawezi kukufanya uwe happy na mwanamke usipokuwa happy maana yake mwanaume ameshindwa kazi ya msingi kabisa katika mahusiano.
Anajiona ni sawa na mwindaji anayerudi mikono mitupu nyumbani baada ya siku nzima ya kuwinda.

Wanawake wengi hutegemea sana mwanaume kuwa source ya furaha zao, huo ni mzigo mzito sana ambao mwanaume anaweza kuubeba.
Pia mwanamke unawajibika kabisa kujipa furaha mwenyewe kwanza, unapochukua jukumu la wewe mwenyewe kuwa mwanamke mwenye furaha na mumeo hujiona amefanikiwa sana hata kama hakufanya lolote kwa furaha uliyonayo na zaidi unapokuwa na furaha unaruhusu moyo wa mumeo kufunguka kirahisi kwako kuliko kuwa jimwanamke lenye uso usio na furaha kama vile ulilazimishwa kuolewa naye.

Pia kulalamika kunafanya mwanamke usiwe attractive, mwanamke unapolalamika kwa kila kitu na kila wakati mwanaume hukuona upo ugly na huvutii kabisa ndo maana wanaume wengi wanawatoroka wake zao kisa mwanamke ni mlalamisha na mwanaume anasema nimeshindwa kujua anataka kitu gani na pia nitawezaje kumfurahisha maana ni kulalamika tu kila siku.


Usiwe Chronic complainer maana kuwe na jua unalalamika, kusiwe na jua unalalamika.

kuwe na mvua unalalamika kusiwe na mvua unalalamika.
uwe na kazi unalalamika usiwe na kazi unalalamika.
Ukiwa mnene unalalamika ukiwa mwembamba unalalamika.
Uwe na mtoto unalalamika usipokuwa na mtoto unalalamika Utaishi na nani?
Nani anataka jitu la aina hii? Jirekebishe
kama umejigundua uko hivyo Mungu ni mwaminifu mwombe akuondelee hiyo tabia na wewe amua kuacha na wafundishe na wengine. Mungu akubariki.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni