Jumatano, 25 Aprili 2012

SAMUEL SASALI A.K.A PAPAA ATISHIWA KUFANYIWA KITU MBAYA AACHA NYUMBA YAKE NA KWENDA KULALA KWINGINE.

Bloger Samuel Sasali anayemiliki blog ya http://www.samuelsasali.blogspot.com, wiki iliyopita alitishiwa na watu wasijulikana kuwa watamfanya kitu mbaya baada ya kutoa post nyingi zinazohusu freemason kwenye blog yake na kwenye kurasa zake za facebook na kufichua baadhi ya mambo ambayo watu wengine hawayajui. akitoa maelezo hayo mbele ya wana bloger wengine walio kutanika kwenye kikao chao cha kwaza. alisema kuwa walianza kumtumia jumbe fupi fupi kwenye inbox yake kama 37 hivi wa kumtishia na za kumtaka aache au la sivyo watamfanyia kitu kibaya na watablock blog yake pamoja na facebook. kilichomshangaza zaidi ni pale watu hao walipomtajia hadi nyumba anayoishi na kumwambia kuwa usiku wake wangeenda kumfanyizia. ili kuepukana nao ilibidi siku hiyo samwel asilale nyumbani kwake alikolala anjua mwenyewe.
Samuel Sasali akiongea na wana Christian bloggers

Bonyeza hapa chini umsikie akitoa maelezo
Samuel Sasali

hayo aliyasema kwenye kikao cha kwanza kilichowakutanisha Christian Bloggers na wamiliki wa tovuti wa Tanzania pamoja na vyombo vya habari ya kikristo ikiwapo TV na radio. kikao hicho kilichoratibiwa na Papa lengo ilikuwa kwanza ni kutambuana na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuufikia ulimwengu kwa technohama. katika kikao hichi kilichohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 15 kilichofanyika Esarp village mlimani city. akiwasilisha alisema wakati umefika wa kukaa pamoja na kufahamiana na kubadilishana uzoefu namna ya kuwafikia watu kwa technohama. naye mwana blogger mkonge aliyeanza siku nyingi ndugu Mbuto naye aliweza kueleza uzoefu wake na changamoto ambazo wana blogger wazopitia, alisema wakati mwingi ni rahisi tu kuona habari ipo kwenye blog lakini kumbe mhusika anaweza kukutana na mazingira magumu, akieleza zaidi alisema yeye wakati anaanza kazi hii ilikuwa ni vigumu hata kuweka picha yake kwenye blog yake kuogopa asijulikane ili isimletee matatizo.
Ndugu Mbuto mwana blogger mkongwe katika blog za kikristo.
wakati mwingine unaweza kupost kitu ukaanza kupigiwa siku za kulaumiwa. hivyo kunakuwa na changamoto katika uandishi wa blog na kubadilika kwa technolojia hivyo kama blogger tunatakiwa kusaidiana namna ya kumiliki blog na kwenda na techolojia alimaliza kwa kusema pamoja na kupasha habari jamii lakini blog inaweza kuwa icome kama ikitumiwa vizuri. pia blogger mwingine Victor naye alielezea uzoefu wake kuwa blog ni sawa na madhabahu katika ulimwengu wa technohama hivyo tunatakiwa kutumia kwa makini ili kuujenga mwili wa kristo, Victor ambaye yeye alikuwa ni blogger bora wa blog za kikristo mwaka, aliweza kusema kuwa tuna kazi ya kuwapasha habari watanzania. alitoa mfano mwaka jana kulikuwa na udhaifu katika upashanaji wa habari katika shindano la kumtafuta Africa Gospel Music awards-Uk akifafanua kuwa Kenya waliweza kutoa washindi 2 lakini ukiangalia washi hao hawanasifa kama waimbaji wetu wa nyimbo za ijili wa hapa kwetu Tanzania kilichotokea ni watanzania kutokujua kwa habari ya shindano hili. hivyo ameomba watanzania sasa kujitokeza kwa wingi ili kupendekeza waimba wa tanzania ambao tunataka waingie kwenye shindano hilo kwa mwaka 2012 kupendekeza majina kumeanza tar 21-04 mpaka 21-05 namna ya kupendekeza fuata linki hii hapo chini.

na baada ya muda wa kupendekeza ukiisha itakuja awamu ya pili ambapo itakuwa kuwapigia kura wale waliopita katika awamu ya kwanza, waliopatikana kutokana na wingi wa mapendezo ya wadau . haya sasa watanzania changamkia nafasi hii ya kupendekeza jina la mwana gospel yeyote unayeona anasifa za kushiriki. 

zifuatazo ni picha mbalimbali za washiriki wa kikao hicho.


James Lue na Martin Malecela

Mussa

King Chavalla

Mdau Prosper Blogger mtarajiwa anayekuja na blog itakayokuwa na  mambo mengi ya wanawake

Erick


Mc D mtangazaji wa ATN alimuwakilisha Dr Venon
Picha ya Pamoja

Samuel na Uncle Jimmy

Mwandishi wa Tanzania daima akiongea na Samuel Sasali.Zifuatazo hapa chini ni blog mbalimbali za kikristo ambazo unaweza kuzitembelea kujifunza mambo mbalimbali ya kiroho.
Ubarikiwe sana
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni