Jumanne, 24 Aprili 2012

KUWA MAKINI NA BIBLIA FEKI ZILIZOINGIA MTAANI

Biblia hizo kwa nje hazina tofauti na biblia tulizozoea kuziona
Biblia ambazo zimechakachuliwa zimezagaa katika nchi yetu ya Tanzania ambazo vitabu vya Daniel, Habakuki na Wafilipi vimeandikwa ndivyo sivyo. Haya yameelezwa na mkurugenzi wa idara ya uanafunzi na maandiko wa kanisa la  TAG Mch Gilbart. Amewataka wakristo kuwa makini na biblia ambazo inasemekana zinaandikwa na wapagani ili kutimiza mkakati wao wa kuelekea kwenye dini na serikali moja Duniani. Alibainisha kuwa kumekuwepo na baadhi ya wapagani hapa nchini ambao huchapisha Biblia zao wenyewe kwa lugha ya kiswahili huku wakichukuwa mfano wa Biblia halisi zilizopo na kubadili baadhi ya vifungu kwa lengo wanalolijua wao la kupotosha ukweli!.
Aliendelea kubainisha huku akiwa na Biblia mojawapo alisema mfano kitabu cha habakuki 2:15 kinasema Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako na kumlevya  pia. Wao wameandika hivi ole wake mtu atiaye sumu kwenye pombe ya jirani yake. Hii wanafanya hivi ili kuhalalisha pombe yaani pombe ni ruksa kunywa ila usimweke mwenzako sumu!. Kitabu cha Daniel 7:7 kinasema nikaona katika njozi ya usiku, na tazama wanyama wanne, mwenye kutisha …. Alikuwa na pembe 10…lakini katika Biblia yao wameandika hivi myama huyo alikuwa na pembe nne ambayo ukiangalia dhahili inapotoshwa makusudi. Wafilipi 3:8 linalosema Naam zaidi ya hayo nayahesabu mambo yote kwa ajiri ya uzuri ya uzuri usio na kiasi wa kumjua kristo Yesu Bwana wangu ambaye kwa ajiri yake nimepata hasara ya mambo yote nikayahesabu kama mavi ili nimpate kristo.wao wameandika hivi Naam zaidi ya hayo nayahesabu mambo hayo kwa ajiri ya uzuri usio na kiasi wa kumjua kristo yesu Bwana wangu ambaye kwaajili yake nimepata hasara ya mambo kama mavi ili nimpate kristo huku neno YOTE likiwa limeondolewa. hii ni sehemu ndogo ya sehemu ambazo zimepotosha na inahitaji mwenye ufahamu mkubwa kuhusu biblia ndiye atakaye weza kujua tofauti yake.
Aidha amewataka wakristo kusoma neno la Mungu kwa bidii na kulielewa na kuwa makini hasa na biblia za kwenye mtandao ambazo mtu anaweza kuedit kwa wepesi ili kupotosha maana halisi ya andiko husika. Na haya yote yanatokea kukiwa na mchakato wa kuunganisha dini mbili kubwa za ukristo na uislam ili kuwa dini moja hivyo tunatakiwa kuwa makini katika huo mchato wao ili usije ukachanganyikiwa na kufuata biblia isiyo sahihi. waandishi wa biblia hiyo wanatumia ujanja wa kutoa neno moja ambalo utakuta linaondoa maana halisi ya sentensi. hivyo watu wa Mungu tuwe makini katika hilo ili tusije tukapotoswa.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Still same Bible!

Bila jina alisema ...

Tunashukuru kwa waraka wako. lakin jinsi ninavyo tambua Biblia ikisha wekewa mikono na padri au mchungaji inatakasika na kuwa Kitabu kitakatifu. Ni kweli jinsi unavyosema na hata biblia yangu naamin ni miongon mwa biblia uliyotaja hapa. lakin kwa uwezo wa roho mtakatifu na ufahamu niliyojaliwa naitambua. ila mim nashauri kitu kimoja, Biblia ya kingereza au biblia za zaman ni nzuri zaidi kwani hazijabadilishwa kama ilivyo kwenye biblia za kiswahili matoleo ya sasa ambayo kila dhehebu linajitahidi kutoa matoleo ya biblia za iman zao na kujukuta tunapoteza kabisa maudhui ya maandiko ya awali. Thanks

Bila jina alisema ...

Tatizo hata huyu anayejaribu kujieleza ana ufahamu mdogo hata wa kuandika Kiswahili chenyewe. Unapotoa taarifa nyeti kama hili hakikisha una taarifa za kutosha la sivyo utakuwa. chombo cha Shetani katika kuwarudisha watu nyuma.