Bunge la nchi ya
Misri liko njiani kupigia kura miswada miwili ya sheria 1 wanaume na wanawake
kuruhusiwa kufanya tende la ndoa na wenzi wake aliyekufa ndani ya masaa 6 baada
ya kufa na 2 kushusha umri wa mwanamke kuolewa hadi miaka 14. ina maana kama mswada huo ukipitishwa
kuwa ni sheria itakuwa ni nchi ya kwanza dunia kuwa na utaratibu ambao
unashangaza watu, wa kufanya tendo la ndoa na mwenzi wako kwa mara ya mwisho ndani
ya masaa 6 baada ya kufa. Mswada huu umekuja baada ya mshemanzi wa Moroko ndugu Zamzami Abdul Bari kusema masuala hayo Mei 2011,
kwamba ndoa bado ni halali hata baada ya
kifo na kuongeza kuwa pia mwanamke ana haki sawa ya kushiriki kufanya ngono na
mume wake aliyekufa. Miaka miwili iliyopita Zamzami alichochea utata huo na zaidi
alisema ni ruhusa kwa wanawake wajawazito kunywa pombe Kwenye nchi hiyo ya Moroko. lakini ikaonekana maoni yake hayo ni
dhaifu huko Moroko na wala hayakufuatwa. lakini cha kushangaza ni kuona kuwa suala hilo limepata
nguvu sana katika nchi ya Misri mwaka huu hata kutaka kulihalalisha kupitia
bunge lao. Ukiachana na sheria hiyo vilevile wamepanga kushusha umri wa
mwanamke mpaka miaka 14 kuruhusiwa kuolewa.
Japo nchi ya Misri ni moja ya nchi ambazo wanaruhusiwa kuoa wanawake
hadi 4 imeushangaza umma kwa hatua wanayoiendea hata hivyo kiongozi wa wanawake
Dr Mervat al-Talawi (National Council for Women .NCW) nchini humo amepinga
kupitishwa kwa sheria hiyo nchini kwao, habari zaidi zinasema amemwandikia barua
spika wa bunge Dr. Saad al-Katatni ili kupinga sheria hizo kupitishwa bungeni maana zinamkandamiza mwanamke. Mambo hayo yanatokea
kipindi kifupi tangu aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak kuondolewa madarakani na nguvu ya umma February
2011. Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na vituko vingi vinavyotokea maana
kuna tukio la kufafana na hili la kijana mmoja huko Thailand kufunga
harusi na maiti mapema mwaka huu soma kwa kufuata link hii http://www.martmalecela.blogspot.com/2012/04/maajabu-ya-dunia-kijana-afunga-ndoa-na.html.
Lakini kwa mtini tujifunde tunapoona matawi kuchanua tujue muda umekaribia, na
mwana wa Adamu atakuja kama mwivi tunatakiwa tujaze taa zetu mafuta na kumngoja
bwana harusi. ubarikiwe
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni