Jumatano, 18 Aprili 2012

JE! WAJUA KUWA KUNA SIKU UTAKUFA?

Pamoja na misele na ujanja ambao mwanadamu anajifanya anao. lakini kumbuka kuwa ipo siku utakufa na kifo kinatupeleka kwenye hatima mbia mbinguni au jehanamu!!!!! lakini Mungu ameweka njia mbili za mtu mwenyewe kuchagua nazo ni uzima na mauti yaani mbinguni au jehanamu. hili halina mjadala ijapo wengi hawataki kukubali lakini ukweli ndo huo. kuna watu wengine wanasema kuwa hakuna jehanamu wala hukumu yeyote. kutokuamini kwako hakutakusaidia kitu wala hakutabadilisha kitu, kama hutakata shauri na kwa kutokuamini kwako ukaenda jehanamu,  nukta moja tu katika jehanamu ya moto itabadili msimamo wako nawe utatambua kwamba uliyoambiwa yalikuwa ni kweli. lakini utakuwa umechelewa mno. itakuwa ni kilio na kusaga meno. kuna mapokeo ambayo ni mapotofu yanayowadanganya watu kuwa ukifa watuwakikuombea basi utasamehewa dhambi huo ni uongo na uzushi kabisa hakuna kitu kama hicho ukifa na dhambi zako hata kama waje dunia nzima wafanya ibada ya aina yoyote ile hawawezi kumshawishi Mungu akusamehu na kukutoa katika jehanamu na kukupeleka mbinguni. hivyo hata kama watu wote duniani wakasema ulazwe mahali pema peponi R.I.P haisaidii chochote mtu anajiweka mahali pema peponi mwenyewe.
wanadamu tumewekewa njia mbili kuchagua uzima au mauti uchaguzi ni wako
mara nyingi watu huwa hawapendi kusimuliwa habari za jehanamu na mbinguni na ndo maana hata baadhi ya watu waabudu shetani wanasema no haven no hell!!!! lakini katika Biblia kitabu cha Dr Luka 16:24-31 ndiyo kitabu peke kinachozungumza habari za watu ambao wapo kuzimu na mara nyingi ninaposoma hapa huwa naona kama vile naangalia sinema vile! inazungumzia watu 2 lazaro na tajiri kuna sehemu mbili na movie hii tunaona maisha ya watu hawa wawili kabla ya kufa ikionyesha tajiri akiponda raha na anasa za kila namna huku Lazaro akipata shida hata kudiriki kula makombo. lakini sehemu ya pili tunaona wote wamekufa sas mambo yamebadilika tajiri yuko kuzimu na Lazaro yuko eneo linaloitwa kifuani mwa Ibrahimu. Tajiri akainua macho na kumwomba ibrahimu amruhusu Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini ili adondoshee tone la maji ulimini mwake ili auburudishe maana alikuwa anteswa sana na moto!! ajabu mtu aliyekuwa na vyote maji kwa haikuwa shida sasa leo anaomba tone la maji!!! majibu aliyoyapata yalimfanya akumbuke na kujua kuwa misa za wafu hazisaidi mtu kwenda mbingu ijapo alikuwa tajiri na alikuwa na watu wengi ambao wangeweza kumwombea lakini Mungu hajibu maombi kama hayo na wanao ombea wafu wanajisumbua na kupoteza muda wao bure sali kabla hujasaliwa. baadae tajiri alimwomba Ibrahimu amruhusu lazaro akawaambie ndugu zake kuwa wasifuate maisha aliyo isha maana nao watakuja huko kwenye moto.
Mtu akiungua kwenye moto
tunaona Ibrahimu akamjibu kuwa kule kuna manabi na watumishi wa hata kama akienda Lazaro hawato msikiliza. ndugu tunapozungumzia jehanamu siyo mzaha ni kweli kabisa watenda maovu (dhambi ) wote watakwenda motoni na wanaotenda mema (watakatifu ) peke yao ndiyo watakao kwenda mbinguni si vinginevyo hivyo kama hutaishi maisha matakatifu ujue jehanamu inakungoja. lakini kwanini uende motoni nawakati neema bado ipo ukiamua sasa unaweza kubadilisha uamuzi wako na kukata shauri la kwenda mbinguni badala ya jehanamu. unaweza kufanya hivyo kwa kusema manenohaya machache tu. sema hivi kwa imani. Bwana Yesu ninakuja kwako mimi mwenye dhambi naomba unisamehe dhambi zangu zote, nitakase nikawe mtakatifu na nisaidie nikaishi maisha matakatibu, niepushe na vishawishi vya shetani, futa jina langu katika kitabu cha hukumi na naomba uandike jina langu katika kitabu cha uzima, asante Yesu kwa upendo wako amina. amini imekuwa kwa imani acha kutenda dhambi tafuta kanisa la watu waliookoka ili upate mafundisho ya kukujenga zaidi kiimani ili ukulie wokovu. au unaweza kuwasiliana na mimi kwa anuani hiyo hapo chini.

MAONI YA MSOMAJI

I live here in Ottawa Canada for the time being and sometimes I am in Boston USA . Yoote ni ubatili mtupu tu .uishi bongo ama ulaya au america nakwambia dunia ni dunia , imejaa ubatili mtupu wala mtu asikutambie na wewe ukayeyuka
 I like so much ujumbe wako -huwa ndio mahubiri yangu na watu hunifikiri nimezidi  wanasema I am too much -but at the end of the day what do you realy want in life ? Uzima wa milele au siyo ?-Kwa bahati mbaya sana Hata injiili za mafanikio zimetumika vibaya hasa mtu anapofikiri ataishi milele na hivyo maombi yanabaki ni kuvunja na kuhahribu kazi za shetani -kwa lengo gani ? ni kweli ili uwe huru na nini ? , halafu? , ili uwe tajiri alafu?  yaani watu hatujui kwamba kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na mengine tutazidishiwa ndio hasa yesu alivyotaka tujue -what we have to seek first -First ? is Kingdom of heaven-mengine yoote hayo yatakuja automatically  -
Kingdom of heaven sio kula na kubywa--Mmh that seem to be even powerful and tougher to some people -Sio kula na kunywa mafanikio nk !! bali ni furaha katika roho mtakatifu -Sasa ikiwa biblia inasema hivi Basi kumbe yatupasa kabisa kujua hapa duniani sio petu hata tuvunje , tuharibu nk nk -NI SAWA sikatai -wala si advocate injili ya umasikini however hakikisha uko tayari kwa safari ya mbinguni first -Yesu alisema ufalme wake sio wa dunia hii and it was true alipaa akaenda .Huko ametukartibisha ili aliko nasi tuwepo. Wapendwa nawaomba sana kuvunja na kuharibu fanyeni na hata mimi hufanya lakini iwe ni kkatika kutafuta ufalme wa Mungu zaidi -Je Jina lako limeandikwa wapi ? ukifa sasa hivi yaani leo hii utakwenda wapi ?
Nadhani kipindi cha kurudia kusambaza tracts kama zamani mitaani zinazouliza "utakaa wapi milele inabidi tuanze upya -wokovu wa sasa hivi wa kupata tu mafanikio yote ila mbinguni ndio inakuwa ziada si wokovu sustainable -inabidi watu tujue prime purpose ya kuokoka ni kuwa na ushirika na mungu kisha kwenda mbinguni -hata kama inaoneekana ni injili ya old school lakini inasaidia kunikumbusha kwamba hapa mimi ni mpiataji. what is your motive ulipoamua kuokoka ? Hakikisha jina lako liko kule mbinguni
tubu dhambi uoke upya kama ulishapotea lengo
ubarikiwe sana mwenye blog hii na kuleta topic hii

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni