Jumanne, 10 Aprili 2012

JAMANI KANUMBA FILAMU YAKE MPYA YA NDOA YANGU ILIKUWA IZINDULIWE MWEZI HUU!!

Marehemu Kanumba the Great alikuwa atoe filamu mpya mwezi huu wa nn,e habari ambazo aliziandika yeye mwenyewe kwenye blog yake kuwa watu waisubiri kwa hamu filamu yake ya NDOA YANGU maskini mipango yake si ya Mungu ndo yametokea hayo yaliyotokea katika filamu hiyo ambayo imeandaliwa na kampuni yake na kuongozwa na yeye mwenyewe kama kawaida yake ndani yake yumo JACK WOLPER kama main character na kuna maneno ambayo aliyaandika yeye mwenyewe yanayosema moja ya vitu tulivyotofautishwa na wanyama na ndege ni Akili ya kujua mema na mabaya,tizama hao ndege na huyo mbuzi hawana akili kabisa lakini wanapendana ndio maana unaona wako pamoja ILA binadamu aliyepewa akili ana roho mbaya sana,katika mafundisho ya YESU KRISTO alisema neno kuu nawapeni PENDANENI.hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima kama huna upendo ni bure,mpende jirani yako kama unavojipenda,upendo haujivuni,hauhesabu mabaya,hautakabari,hauhusudu.....nk,1WAKORINTHO 13.Mungu ana akili sana kutuumba kwa mwili huu wa nyama laiti kama angetuumba kwa vioo au sightmirror ili uweze kuona mwenzako anakuwazia nini?anakufanyia nini?anapanga nini juu yako ungekuta ni heri ukaishi msituni na wanyama wakari kuliko kukaa na binadamu,katika tafiti zangu nimegundua kuna dawa mbalimbali mfano ya kichwa,homa,nk Lakini dawa ya Chuki na roho mbaya hakuna,,kama hiki kingekuwa kipindi kama kile cha zamani za Sodoma na Gomora au cha Nuhu ambacho Mungu alikuwa akiadhibu hapo hapo watu wengi sana wangeumbuka hasa wale wanaojifanya wasafi usoni lakini rohoni ni tofauti,Mungu atusaidie sana hasa sisi vijana tujue kusimama katika ukweli na uwazi,tuubebe upendo wa dhati toka rohoni huku mdomoni tukitamka amani ya kweli impendezayo Mungu ili watoto wetu waje watuenzi kwa mazuri na dunia ijivunie uwepo wetu.
Kazi ya kutengeneza filamu ikiendelea


Marehemu Kanumba The Great na wooper wakiigiza
Marehemu kanumba akiwaelekeza Msungu na Wooper
Zakayo camera man wa Marehumu Kanumba akiwa kazini

mpaka sasa hakuna taarifa zozote ambazo zimetolewa kuhusiana na kuitoa filamu hiyo nafikili mpaka msiba utakapoisha ndipo mambo mengine ya kiofisi yataendelea ikiwapo kutoa filamu hiyo ambayo najua itauzika sana na itapata umaarufu mkubwa maana ndiyo itakuwa ya mwisho iliyokamilika inayoonyesha umahili wa kipaji alichopewa na Mungu

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni