Jumanne, 10 Aprili 2012

MAZISHI YA KANUMBA SIJAWAHI KUONA !!!!!? UMATI MKUBWA WA WATU!!!!!


Nimewahi kushuhudia misiba mingi ya watu maarufu na viongozi lakini ukweli sijawahi kuona msiba uliogusa mioyo ya watu wengi kama huu wa Kanumba, watu wengi wamehuzunika na si hapa Tanzania tu bali hata nchi zinazozunguka nchi ya Tanzania Afrika nzima na hata Ulaya na Marekani. Mimi binafsi sikujua kama Kanumba alikuwa maarufu kiasi hiki na sipati picha kama Mungu angempa miaka mingine 28 ingekuwaje??!! Umati ambao ulianza kukusanyika kuanzia siku aliyokufa na kufanya hadi vituo vya radio kutangaza kuwa watu wasiendelee kwenda nyumbani kwake ambako kulisababisha hata barabara kufungwa na kusababisha hata polisi kulazimika kuweka ulinzi mkali kuanzia nyumbani kwake. Lakini kilichotia fola ni umati ambo umejitokeza kumuaga na kusababisha hata baadhi ya barabara kufungwa leo wakati wa shughuli za kumuuaga watu wengi wamezimia hata kusababisha hata viwanja ambavyo vilidhamiwa vitafaa leaders kuwa ni mahali padogo hata kuhatarisha usalama wa watu na kusababisha ratiba ya mazishi kubadilishwa ili kuondoa msongamano wa watu ambao nao ungeweza kusababisha maafa mengine. Ukiachilia umati huo wa watu lakini kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakifuatilia tukio hilo kwa njia ya clouds TV/ radio na Internet ili wate wanje ya Tanzania waweze kushuhudia tukio hilo.
Jeneza la kanumba


Wasani wa filam wakiwa wamebeba jeneza la the great Kanumba

Jeneza la The Great kanumba

Umati wa watu wakiwa leaders club
Umati huo umesababisha kuahilisha zoezi la kuaga mwili wa marehemu ambao ilikuwa ufanyike kuanzia saa 12:00-15:00 hivyo kulazimika kuuondoa mwili wa marehemu na kuupeleka katika makaburi kwa mazishi pamoja na hivyo bado umati mkubwa uliendelea kumiminika bila kujua kuwa ratiba inebadilika. ukiacha umati huo wa watu kulikuwa na viongozi wengi mbali mbali wakiongozwa na makamu wa Rais Mohamed Bilal ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi. tukio hilo limesababisha madaladala kubadilisha root zao na kuelekea leaders club na kupanda kwa nauli kwa baadhi ya magari. pamoja na hayo polisi walikuwa na kazi ya ziada na ilibidi watumie hata bakora ili kuhakikisha usalama unatawala. mazishi bado yanaendelea tutaonana baadae.



KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela

Hakuna maoni: